TCAA:HAIKUWA AJALI NI MAJARIBIO




Kulia ni Afisa uhusiano TCAA,Yessaya Mwakifulefule, kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege kutoka TCAA), Flora Alphonce wakizungumza na Waandishi Wa habari Leo jijini Dar es salaam, 



waandishi Wa habari Wa Vyombo mbalimbali wakifuatilia taarifa hiyo. 

*******


MAMLAKA ya Usafiri wa Anga(TCAA)imewatoa hofu Watanzania kuhusu kuwepo kwa ajali ya Ndege aina ya Embraer 120 iliyokuwa imebeba Abiria 25 iliyoanguka katika kijiji cha msufini kata ya Mbezi wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kuwa haikuwa ajali bali lilikuwa ni Zoezi la kujiweka utayari kwa ajili ya kupambana na majanga ya Ajali za ndege pindi yakitokea.

 

Akizungumza na waandishi kwa niaba ya Mkurugenzi wa TCAA,Hamza Johari,Afisa uhusiano TCAA,Yessaya Mwakifulefule,amesema zoezi hilo ambalo lengo lake ni kupima uwezo na utayari  kama nchi kukabiliana na matukio ya utafutaji na uokoaji wa ndege zinazopata ajali kwenye nchi kavu au majini na pia vyombo vya majini.

 

Aidha,Mwakifulefule,amesema zoezi hilo limeandaliwa na TCAA,shirika la uwakala wa meli nchini(TASAC),Mamlaka ya Usafiri wa Baharini upande wa Zanzibar(ZMA) pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama.



Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege kutoka TCAA), Flora Alphonce amesema zoezi hili limehusisha Vyombo mbalimbali vya uokoaji ambavyo ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Zimamoto, Shirika la Msalaba Mwekundu, TANAPA , TASAC, Jeshi la Polisi nk. ili kujiweka tayari kipindi wanapopata ajali halisi katika anga la Tanzania.

0/Post a Comment/Comments