Mamlaka ya Hali ya HewaTanzania (TMA) imesema hadi kufikia sasa inaonyesha imefikia asilimia 90 ya kuwepo kwa mvua za El nino hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Pia imesema El Nino inatarajiwa kuwepo katika kipindi cha mvua za msimu wa vuli zitakazoanza kunyesha Oktoba hadi Desemba mwaka huu ambazo zitasababisha athari katika maeneo mbalimbali nchini.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Meneja wa Utabiri wa TMA, Dk Mafuru Kantamla amesema kuwa katika kipindi hiki cha Kipupwe ilitarajiwa kuwa El Nino itaanza kujitengeneza msimu huu na tayari imeanza kujitengeneza.
Dkt Kantamla ameyataja maeneo ambayo yanatarajiwa kuathirika na mvua za El nino kuwa ni mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.
Hata hivyo Dkt Kantamla amesema kunapokuwepo El nino " kunategemewa ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo ya nchi" lakini ongezeko hilo linategemea na msimu, na kwamba limetokea katika msimu upi ili kubainisha athari zake.

Post a Comment