NA MUSSA KHALID
Wanaharakati wa maji Mkoa wa Dar es salaam wamesisitizwa kuendeleza kampeni ya utunzaji wa rasilimali maji ikiwa ni pamoja na kuingiza suala la kijinsia katika kampeni zao.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mshauri Mkuu wa wanaharakati wa maji safi na maji taka na jinsia Bi.Gema Akilimali wakazi akizungumza katika kikao cha kujadili mpango mikakati ya namna ya kutunza na kuhifadhi rasilimali maji.
Akilimali amesema kuwa mpango mkakati ambao umepangwa na wanaharakati hao kupitia Shirika la Shahidi wa Maji utakwenda kuamsha morali ya kuwakumbusha wafanya maamuzi kuweza kutekeleza wajibu wao katika kufanya utatuzi wa changamoto ya rasilimali za maji katika maeneo mbalimbali.
"Ushauri wangu kwa Wanaharakati wa Maji nikuendeleza kampeni za maji Kwa kuunganisha ushirikiano kwa mapana yake kwani itakuwa na tija na itanyanyua wengine kushiriki mapambano ya rasilimali maji"Bi Akilimali
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa wanaharaki wa maji kupitia shahidi wa Maji na TGNP Mtandao Tabu Ally amesema malengo yao kuitumikia jamii ili iweze kupata maji na hivyo kuwa na maisha bora.
Miraji Awadhi Simba ni Katibu Msaidizi wa wanaharakati wa maji Mkoa wa Dar es salaam amesema watahakikisha wanafanya muendelezo wa ufuatiliaji wa maji safi na maji taka ili kueipusha jamii kuathirika na maji hayo.
Ikumbukwe kuwa Shirika lisilokuwa la kiserikali la shahidi wa Maji -SwM limekuwa likiwakumbusha watanzania kuchangia utunzaji na rasililimali za vyanzo vya maji ili kusaidia kuepukana na changamoto ya ukosefu wa Maji katika maeneo mbalimbali nchini.





Post a Comment