UMEME WA BWAWA LA NYERERE KUWASHWA JUNI 2024


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Maharage Chande akizungumza katika kikao kazi na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF kilichofanyika leo Alhamisi Julia 27,2023 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) Deodatus Balile akitoa shukurani zake na kupongeza maboresho ya utendaji kazi wa shirika hilo kwa kipindi cha Miaka ya hivi karibuni.


 

Wahariri na waandishi wa habari kutoka Vyombo vya habari Mbalimbali mapema Leo 

********

UJENZI wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere unatarajiwa kukamilika Juni, mwakani 2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amewaambia wahariri wa habari leo Alhamisi, Julai 2023 kuwa mradi huo kwa sasa umefika asilimia 90.

Kwa mujibu wa Chande, kukamilika kwa bwawa hilo kutaongeza ufanisi  na changamoto ya umeme nchini itabaki kuwa historia.

Chande amesema ujenzi wa bwawa hilo litakalozalisha megawat 2100 umetumia kiasi cha Sh6.5 trioni fedha ambazo ni nyingi kuliko miradi yote nchini zilizotolewa na Serikali.

“Ujenzi wa bwawa hili ukikamilika tutakuwa na uwezo wa kuunganisha wateja wa nyumba zote nchini, “ amesema Chande na kuongeza kuwa kwa matumizia ya sasa ni  megawati 1400 pekee.

Amesema asilimia 50 kwa sasa ni wateja wa majumbani na iliyobaki inatumiwa na wateja wakuwa wa viwanda.

Naye Mwenyekiti wa Juiwaa  la wahariri (TEF ), Deodatus Balile  amelipongeza shirika hilo kwa maboresho wanayoendelea kufanya katika utoaji wa huduma zake kwa wateja na ameshauri mfumo wa utendaji wa shirika hilo utumike pia katika taasisi zingine za umma.

0/Post a Comment/Comments