Version Conflict: TIGO YAKABIDHI MILIONI TANO YA CHAWOTE



Meneja kanda ya Kinondoni Beatrice kinabo kulia akimkabidhi Mshindi wa kwanza kutangazwa wa CHAWOTE aliyejishindia shilingi milioni Tano kutoka Dar es salaam Kinondoni, Upendo Konya leo jijini Dar es salaam 
Mshindi wa kwanza kutangazwa wa CHAWOTE aliyejishindia shilingi milioni Tano kutoka Dar es salaam Kinondoni, Upendo Konya,akiwa ameshikilia Mfano wa Hundi 


Wananchi na wadau mbalimbali waliojitokeza viwanja hivyo kushuhudia mshindi akikabidhiwa Mfano wa hundi ya milioni tano 


**********

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo Tanzania, leo imemkabidhi mshindi wa wa kwanza kiasi cha Shilingi milioni Tano wa Kampeni ya CHAWOTE, 

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, wakati akimkabidhi mshindi Huyo wa Cha wote, Meneja kanda ya Kinondoni Beatrice kinabo, amesema kuwa kupitia kampeni hiyo,washiriki ambao watatumia huduma za tigo mara kwa mara kwa kukunua vifurushi,muda wa maongezi kwa kupitia lipa namba,tigopesa na kufanya huduma za kampuni hiyo wataweza kuingia kwenye droo na kushinda.

Aidha amesema kuwa katika kampeni hiyo itachukua siku tisini ambapo itakuwa na washindi 28896.

Kwa upande wake mshindi wa kwanza kutangazwa wa CHAWOTE aliyejishindia shilingi milioni Tano kutoka Dar es salaam Kinondoni, Upendo Konya, amesema kuwa ameweza kushinda kiasi hicho ambacho kitaenda kumsaidia kukuza kazi zake za ujasiriamali ambazo ndiyo anazozifanya ikiwemo mitindo na ufundi cherehani.





0/Post a Comment/Comments