Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza katika kuadhimisha siku ya Utamaduni wa Ujerumani na Mtanzania ambayo yamefanyika katika Kijiji cha Makumbusho kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam yaliyohudhuriwa na vijana kutoka Bavaria nchini Ujerumani na Watoto wenye uhitaji maalum kutoka eneo la Manzese.
Mwanzilishi wa Taasisi ya Youth Crossing Boundaries, Father. George Rupperecht kutoka MJI wa Bavaria nchini Ujerumani akizungumza katika kuadhimisha siku ya Utamaduni wa Ujerumani na Mtanzania ambayo yamefanyika katika Kijiji cha Makumbusho kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam
Baadhi ya zawadi mbalimbali ambazo Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akimpatia Mwanzilishi wa Taasisi ya Youth Crossing Boundaries, Father. George Rupperecht kutoka MJI wa Bavaria nchini Ujerumani katika maadhimisho hayo sambamba na kuwazawadia vijana Hao wa Ujerumani.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga (kushoto) Pamoja na Mkuu Kituo Cha Utamaduni Cha Ujerumani Nchini Tanzania Cha Goethe Institute Nassori Nascov (Kulia) wakiwa katika maadhimisho ya siku ya Utamaduni wa Ujerumani na Mtanzania ambayo yamefanyika katika Kijiji cha Makumbusho kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam
Picha ya Pamoja Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga Pamoja na vijana kutoka Bavaria Ujerumani wakiwa na Kiongozi wao Mwanzilishi wa Taasisi ya Youth Crossing Boundaries, Father. George Rupperecht (picha na Mussa Khalid)
....................,.
NA MUSSA KHALID
Nchi ya Tanzania kwa Ushirikiano na nchi ya Ujerumani kupitia Taasisi zake za Makumbusho ya Taifa zimeunganisha tamaduni na kuweka Jamii pamoja Ili kujifunza na kubadilishana uzoefu.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya Utamaduni wa Ujerumani na Mtanzania,Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema kuwa kujifunza Utamaduni ndio msingi wa amani,Umoja na Maendeleo kwa Taifa.
Aidha Dkt Lwoga amewataka Watanzania kuendelea kuzitunza na kuzithamini Tamaduni za nchi kwani ndio kielelezo muhimu na utambulisho katika Mataifa mbalimbalia Duniani.
Ameeleza kuwa Muungano kati ya Tamaduni za Ujerumani na Tanzania unasaidia kuendelea kuunganisha Umoja na jamii kuzifahanu Tamaduni za Mataifa hayo mawili.
"Tanzania ni wamoja kutokana na mashirikiano katika Tamaduni mbalimbali ambazo zote huunganishwa na lugha ya Kiswahili hivyo ni vyema Jamii ikaendelea kuhifadhi Amesema Dkt Lwoga
Kwa upande wake Mwanzilishi wa Taasisi ya Youth Crossing Boundaries, Father. George Rupperecht kutoka MJI wa Bavaria nchini Ujerumani amesema lengo ni kuwapatia haki ya elimu Watoto wenye uhitaji maalum kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka vyuo vikuu.
Naye Mwalimu Joanitha Kichemi ambaye ni Mratibu wa taasisi ya Youth Crossing Boundaries Foundation iliyopo kata ya Manzese inayojishughulisha na kuwalelea watoto wanaoishi Kwenye Mazingira hatarishi amesema lengo lao ni kuwainua watoto Ili waweze kutimiliza ndoto zao.
Pi ameishauri Jamii kuwa na moyo wa kujitolea kuwasaidia wenye uhitaji Ili nao wapate furaha kama walivyo wengine jambo ambalo litasaidia waweze kufanikisha malengo yao.
Naye Mkuu Kituo Cha Utamaduni Cha Ujerumani Nchini Tanzania Cha Goethe Institute Nassori Nascov amesema wamekuwa wakijikitabzaidi katika kufundisha lugha ya Kijerumani Ili kuwarahisishia watanzania katika Masuala ya kibiashara Kwa inaunganisha na kuwa kama daraja.
Baadhi ya wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali Amour Rajab kutoka shule ya Msingi Ukombozi Pamoja na Debora Makungu kutoka shule ya Msingi Uzuri wamesema kuwa Taasisi hiyo imewasaidia kuwatoa katika huzuni kwani wanawapatia elimu.
Maadhimisho hayo yamewajumuisha Watoto wenye uhitaji maalum kutoka eneo la Manzese jijini Dar es salaam wanaofadhiliwa na taasisi ya Youth Crossing Boundaries Foundation.









Post a Comment