Waandishi wa Habari wakifuafilia kwa umakini mutant baina Yao na Waziri Kivuli wa Nishati wa Chama cha ACT wazalendo Isiaka Mchinjika mapema leo jijini Dar es salaam.
( PICHA NA JAMES SALVATORE)
CHAMA cha ACT wazalendo kimeiomba Serikali kupunguza matumizi ya Mafuta kwenye Magari yake , na badala yake kutumia Gesi kwenye Magari hayo ili kupunguza Gharama za uendeshaji wa Serikali na Uhaba wa Dola nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema Leo jijini Dar es salaam, Waziri Kivuli wa Nishati wa Chama hicho,Isiaka Mchinjika amesema kuwa Endapo Serikali itatumia gari zenye mfumo wa gesi itapunguza gharama na uhaba wa Mafuta hayo hivyo kuepukana na uhaba wa dola na changamoto zinazotokana na nishati hiyo.
Waziri kivuliwa Nishati Mchinjika alisema sambamba na magarihayo pia Magari ya Mikoani pia yaweze kutumia Mitungi ya Gesi.
Alisema Nivyema Benki kuu kuwasisitiza wazalishaji wa ndani kutumia Shilingi badala ya Matumizi ya Dola katika Manunuzi.
"Ili kudhibiti Mahitaji ya Dola ya shilingi bilioni140 kwa siku"Aliongeza Mchinjika.
Mchinjika alisisitiza nivyema Serikali kuongeza thamani ya Mazao ya kilimosambamba kuongeza Urali wa fedha Dola bilioni 4.







Post a Comment