Timothy Marko
Waziri Uwekezaji Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa kitilya Mkumbo amezindua hatifungani ya "kijani Bond" ya Shilingi Bilion 780 ya Benki ya CRDB kukubiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi.
Akizindua hatifungani hiyo jijini Dar es Salaam Profesa kitilya Mkumbo amesema kuwa hatihiyo niya kwanza katika ukanda wa nchi za jangwa la Sahara .
"Hatifungani hii ya kijani bond itawezesha kukamilika kwa Miradi ya Nishati na Maji,ilikuhamasisha Uhifadhi wa Mazingira".Alisema Waziri wa Uwekezaji Profesa Kitlya Mkumbo.
Profesa Mkubo alisema Benki ya CRDB imekuwa ya kwanza nchini kutoa hatifungani katika uhifadhi wa Mazingira ambayo inachangamkiwa Duniani.
"Serikali katika kuweka Mazingira rafiki katika kuwezesha hati fungani ya kijani utachochea Maendeleo ya kiuchumi"Aliongeza Waziri Professa Mkumbo.
Awali,Mkurugenzi wa Benki CRDB Majid Nsekela ameishukuru Taasisi ya Masoko ya Mitaji CMSA kwa kuuza hati hiyo ya barani Afrika.
Alisema Hatifungani hiyo itasaidia kufanya utatuzi wa ukamilikaji wa baadhi Miradi ya Maji na Nishati ambapio thamani hatifungani Dola Milioni 300 sawa shilingi bilioni 80.

Post a Comment