BENKI YA MAENDELEO KUCHANGIA Mil.200 WATU WENYE USONJI.


 .........................

Timothy Marko.

KATIKA kuhakikisha Afya ya Mama na mtoto na watoto njiti inaimarika,Benki ya Maendeleo imezindua matembezi ya hisani kwa kujili kusaidia vifaa vya Afya na watoto wenyetatizo la usonji.

Matembezi hayo yanayoanzia katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam hadiViwanja vya Farasi jijini Dar es salaam yanalenga kukusanya Shilingi milion 200 kwa ajili ya watoto wenye usonji.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za benki hiyo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo Dk Ibrahim Mwangalaba amesema hatua hiyo imefuatiwa nabenkihiyo kupata faida ya Shilingbilion144 na kufikisha wateja 600 .

"Shilingi Milion200 vitatumika kununua vifaa vya watoto njiti".Alisema Mwangalaba.

Mkurugenzi wa benki ya Maendeleo Mwangalaba alisema kuwa mbio hizo zinatarajiwa kuanza Septemba 2 katika ofisi za Makao makuu yabenki hiyo hadi viwanja vya Farasi jijini Dar es Salaam.

Naye Mkuu wa wilaya ya ilalaEdward Mpogolo amesemakuwa Benki yaMaendeleo imekuwa mdau mkubwa katika ukuajiwa sekta ya ajira nchini.

Alisema katika kipindi2022/23imeweza kuwa na watumishi 114 huku tangia ianzishwe benki  hiyo awali ilikuwa na watumishi 14 tu.

"Benki hii imekuwa ikitoa Mikopo kwa wamachinga ilikuweza kukuza biashara zao".Alisema Mpogolo.

0/Post a Comment/Comments