TCU YAWATADHALISHA WANANCHI NA "VISHOKA".

........................

Timothy Marko 

TUME ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) imewataka waombaji wa Shahada ya kwanza ya Mwaka wa masomo 2023/2024 kuweza kufanya udahili kuanzia leo hadi Septemba6 2023.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo nchini Profesa Charles kihampa amesema tume hiyo imewataka waombajwote ambao hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa wawezekutuma maombi yao tena katika vyuo wanavyovipenda.

"Tume inawasisitiza waombaji wote kuzingatia taratibu za udahili kama ilivyo elekezwa kwenye wavuti yetu www.tcu.go.tz" Alisema katibu Mtendaji Prof.Charles Kihampa.

Profesa kihampa alisemawaombaji wa udahili wa Shahada ya Kwanza wanakumbushwa masuala ya udahili yanafanyika katika chuo husika.

Alisema kwa wale watapata changamoto katika kujithibitisha waweze kufuata Miongozo kwa taratibu zilizowekwa.

"TCU inawaasa wananchi kuweza kuepuka kutapeliwa na wanaojiita mawakala washauri wanatoa huduma ya kujiunga na vyuovya Elimu ya juu hapa nhini"Aliongeza Dk kihampa.
 

0/Post a Comment/Comments