BODI YA RUWASA YATEMBELEA MRADI WA MAJI MBANGAMAWE SONGEA


........................................

Bodi ya RUWASA imeendelea na ziara yake, leo imeingia Mkoani Ruvuma na kutembelea Chombo cha watoa huduma ya maji ngazi ya jamii Mkilima na kisha tutembelea Mradi wa Maji Mbangamawe Wilaya ya Songea Vijijini.

Wakisoma taarifa ya Chombo hicho cha kutoa huduma katibu wa chombo amesema chombo kinakusanya wastani wa shilingi milioni  6.5 na matumizi ni shilingi milioni 2.7 kwa mwezi. 

Kwa upande wao wananchi wa Mbagamawe wameishukuru serikali kwa kuwajengea mradi mzuri wa maji kwani hapo awali walikuwa wanapata maji kwa gharama kubwa jambo ambalo lilizorotesha shughuli za maendeleo na hata ujenzi.

Katika kudhihirisha furaha yao wananchi wametoa zawadi ya mbuzi wawili, Mkungu wa ndizi na gunia la mahandi kwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya RUWASA.

0/Post a Comment/Comments