*****
Na Richard Mrusha, Mbeya
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) umetekeleza Mradi mkubwa wa ghala la kuhifadhia chakula Tani 21,000 katika Wilaya ya Sumbawanga na umegharimu Dola za kimarekani Mil.6.1.
Mradi huo ni wa teknolojia ya kisasa na unatekelezwa katika Mikoa nane ya Tanzania ikiwemo Mikoa ya Nyanda za Juu kusini,Songea, Songwe Makambako, Sumbawanga, Katavi, Shinyanga Manyara na Mkoa wa Dodoma.
Mhandisi wa mradi huo Haruna Kalunga amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari leo Agost 4,2023 walipotembelea banda la Wakala wa majengo Tanzania TBA Kwenye sherehe za maonesho ya kimataifa ya kilimo Nane Nane 2023.
Mhandisi Kalunga amebainisha kuwa mradi wa ghala la kuhifadhia chakula Sumbawanga umeanza kutekelezwa mwezi Januari 2020 na umekamilika mwezi Machi 2023 na umeanza kutumika kwa kuhifadhi mazao ya chakula kwa Wakulima.
"Mradi huo ni wa teknolojia ya kisasa, na unatunza chakula cha walicholima wakulima Tani 21,000 na lengo kuu la mradi huo kutekelezwa kwa Mikoa 20 lakini kwa sasa tumeanza na Mikoa Nane," amesema Wakala wa majengo Tanzania mhandisi Haruna Kalunga.
Aidha Mhandisi Kalunga alitumia nafasi ya wanahabari hao kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo na kufika katika banda la TBA ili kujua mambo mbalimbali ikiwemo gharama za ujenzi pamoja wa nyumba za makazi na taasisi za serikali kwa ghalma nafuu.
Mwisho.

Post a Comment