NA MUSSA KHALID
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini imewasisitiza wanasiasa kuendelea kuwa wazalendo katika ufanyaji wa siasa zao ikiwa ni pamoja na kulinda mtaji wa kisiasa kwa mustakabali wa Taifa
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Fransic Mutungi wakati akizungumza katika kikao Maalum Cha Baraza la Vyama vya siasa na Viongozi wa Dini ili kujadili na kufanya tafakuri ya siasa wanazozifanya ziweze kuwa na tija mwa nchi.
Aidha Jaji Mutungi amesema pia kikao hicho kimefanyika kwa utekelezaji mahususi wa Baraza la Vyama vya siasa kwa kuangalia changamoto zilizopo katika mikutano ya hadhara inayoendelea kufanya na vyama vya siasa tangu mikutano hiyo iliporuhusiwa.
"Ofisi ya Msajili sio kituo Cha Polisi na wala sio malaika hivyo musiogope kukutana na sisi kwa ajili ya mazungumzo na kuturekebisha tunapokosea kwani msemo wa waswahili unasema tunajenga Nyumba Moja tusigombee fito"amesema Jaji Mutungi
Profesa Alexander Makulilo ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam amewasilisha mada Kuhusu Vyama vya siasa kutumia Viongozi wa dini katika shughuli za kisiasa amesema uhusianao uliopo kati ya dini na siasa ni changamano lakini katika nchi yetu imewekwa sheria ili kuratibu mchangamano huo
Kwa upande wao baadhi ya Viongozi wa Dini ambao wamehudhuria katika mkutano huo akiwemo Shekh Mussa Yusuph Kundecha Amiri Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya za Taasisi za Kiislamu Tanzania amesema kuwa siasa na dini ni vigumu kutofautisha kwani yote ni Maisha ya Jamii,hivyo ni vyema Kiongozi wa dini akaepuka kuwa mshabiki wa chama au kuhubiri Juu ya Chama Fulani Cha siasa.
Naye Padri Florence Rutaiwa kutoka Baraza la Maskofu Tanzania ni vyema viongozi wa dini wakaepuka kuwa mshabiki wa Chama au kuhubiri juu ya Chama Fulani cha siasa ili kuondoa migongani kwa jamii.
"Kama Viongozi wa dini ni vyema tukajua mipaka yetu katika changamano na siasa kwani dhamira yetu hatupaswi kuleta mafarakano katika nchi yetu kwa kushirikiana na wanasiasa"amesema Padri Rutaiwa
Hata hivyo viongozi wa vyama vya siasa wamesisitizwa kutumia fursa ya kutoa maoni yao wakati wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa,tume ya uchaguzi il kuendelea kuimarisha taasisi hiyo.


Post a Comment