Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam Ojambi Masaburi akizungumza katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani cha kupitisha na kujadili taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2023 ambacho kimefanyika Leo katika Ukumbi wa Anatoglo.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Ilala Mbala Shitindi akizungumza katika kikao Baraza la Madiwani cha kawaida cha kupitisha na kujadili taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2023 ambacho kimefanyika Leo katika Ukumbi wa Anatoglo.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Tabu Shaibu akizungumza katika kikao Baraza la Madiwani cha kawaida cha kupitisha na kujadili taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2023 ambacho kimefanyika Leo katika Ukumbi wa Anatoglo.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani ambao wamehudhuria katika kikao cha Baraza la Madiwani kawaida cha kupitisha na kujadili taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2023 ambacho kimefanyika Leo katika Ukumbi wa Anatoglo.
...................
NA MUSSA KHALID
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,limewaelekeza wataalamu na watendaji wa jiji hilo kwenda kuweka mchakato wa kuhakikisha wanashughulikia suala la Bima ya Afya ili madiwani waweze kunufaika na mfuko huo.
Hayo yamejiri katika kikao cha kawaida cha kupitisha na kujadili taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2023.
Akizungumza katika kikao hicho Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam Ojambi Masaburi amesema kuwa kutokana na changamoto ambayo wamekuwa wakikumbana nayo katika baadhi ya vituo vya afya wameamua kuazimia hilo kwani litasaidia pia kuongeza ukusanyaji wa mapato.
‘Tunapozungumza ufanyaji kazi watendaji kazi ni waheshimiwa madiwani na wakuu wa Idara hivyo ni lazima umlinde mfanyakazi wako anayefanya kazi kwenye hili tumekubalina wataalamu na watendaji wakafanye mchakato wa kulishughulikia suala la bima ya Afya’amesema Masaburi
Aidha kuhusu ukusanyaji wa mapato katika jiji hilo Naibu Meya Masabauri amesema kuwa wamepanga kukusanya zaidi ya mapato zaidi ya asilimia 40 ili kuongeza miradi zaidi zikiwemo Hospitali za wilaya kama walivyokubalina kwenye baraza.
Awali akitoa maelekezo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Ilala Mbala Shitindi amelieleza Baraza la Madiwani kuwa kuhusu Vifurushi ambavyo havipo kwenye kifurushi cha muhusika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wanajukumu la kuingia Mkataba na Mwajiri ili kuweza kubadilisha kifurushi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Tabu Shaibu ametumia fursa hiyo kueleza kuwa jiji hilo limeendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kisekta ikiwemo ya elimu pamoja na huduma za jamii.
Amesema kuwa Halmashauri hiyo imeamua kuanzisha ofisi za kanda ili kuendelea kuongeza ufanisi kwa ukaribu jambo ambalolitasaidia kuongeza mapato kwa wingi katika jiji hilo.
Hata hivyo katika kikao hicho
kiliweza kupitia taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Fedha na Utawala, Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii, Kamati ya Mipango Miji na Mazingira pamoja na Kamati ya Kuthibiti UKIMWI kwa kipindi cha Aprili hadi Juni 2023 lengo likiwa ni kujiridhisha juu ya utendaji kazi wa kamati hizo.
Sambamba na hilo, Kamati ya Mipango Miji na Mazingira kupitia Divisheni ya Miundombinu Kamati imeweza kusimamia ukaguzi na utoaji wa vibao vya ujenzi vipya 182 na vibali 74 vya ukarabati huku Idara ikitoa notisi 44 kwa watu waliojenga bila ya kuwa na vibali vya ujenzi pamoja na kutatua migogoro ya Ardhi na mipaka katika Mitaa na Kata mbalimbali za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.



Post a Comment