
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na afisa mtendaji mkuu wa baraza la taifa la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Tanzania (NACOPHA) Deogratius Rutatwa wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amebainisha kuwa baraza hilo kwa kushirikiana na ofisi ya waziri mkuu wamedhamiria kufikia maambukizi sifuri ya virusi vya ukimwi.
Amebainisha kuwa kwa sasa takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watu wanaojua kuwa wanaishi na virusi vya ukimwi imefikia asilimia 96, watu waliopima na wanaoendelea na matibabu imefikia asilimia 98 huku ambao tayari virusi vyao vimefubazwa ikiwa imefikia asilimia 97.
Amesema kuwa baraza hilo kwa kutambua umuhimu wa mapambano dhidi ya maambukizi ya ukimwi wameandaa tamasha lenye lengo ya kukusanya rasilimali fedha zitakazowezesha afua mbalimbali za mapambano hayo linalotarajiwa kufanyika mnamo Agosti 11 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa dar es salaam Albert Chalamila.
Aidha amesema rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mdahalo wa kitaifa unaolenga kujenga ubia kati ya wadau na jamii kuhakikisha kwamba wanakua na mkakati endelevu wa kuhakikisha kwamba matokeo yaliyopo katika muitikio ya UKIMWI yanaendelezwa na kufikia malengo ya kimataifa ya 03 ifikapo mwaka 2030.
Mdahalo huo ambao utaanza mwezi Desemba 11, Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali, imeandaliwa na Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania ikishirikiana na Baraza la watu wanaoishi na VVU chini ya uratibu wa ofisi ya waziri mkuu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uraghibishi na Habari (TACAIDS), Jumanne Isango amesema wanataka ifikapo mwaka 2030 wawe wamemalza kabisa tatizo la UKIMWI hii ni kupitia njia ya kukusanya rasilimali ikiwemo mfuko wa kudhamini udhibiti UKIMWI ambao serikali, wananchi, Taasisi na wadau mbalimbali kutoka nje wanaweza kuchangia
Naye mwenyekiti wa vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi Pudenciana Mbwiliza amesisitiza kuwa wadau hawana budi kuungana kwa pamoja ili kuhakikisha nguvu kazi ya taifa inalindwa dhidi ya maambukizi mapya ya ukimwi ili kuongeza ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo huku akiwaasa waathirika wanaojificha kujitokeza kwa jamii na hivyo kuwa sehemu ya mapambano dhidi ya virusi hivyo.
Mbwiliza, amesema wao kama Baraza wamechukua jukumu la kuwa sehemu ya wengine wengi ambao bado hawajaweza kujitokeza hivyo wanaamini kupitia mdahalo huo wa kitaifa vijana wengi ambao wanaendelea kujificha nje watakuwa ni sehemu ya mabadiliko nchini.








Post a Comment