NA MUSSA KHALID
Takriban Makampuni ya bidhaa za Afya zaidi 105 Duniani yanatarajiwa kushiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Afya ili kuleta fursa za watoa huduma katika sekta za afya kuonyesha bidhaa zao wanazozalisha.
Imeelezwa kuwa maonyesho hayo yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Agost 24-26 mwaka huu ni ya pili kufanyika nchini ambapo makampuni kutoka mataifa la India,Kenya,Yemen,China,Algeria pamoja na mwenyeji Tanzania.
Akizungumza jijini Dar es salaam Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) Fadhili Hezekiah amesema kuwa ni vyema watanzania wakashiriki katika maonyesho hayo ili waweze kujifunza uwekezaji unaofanywa na wawakezaji.
Awali akizungumzia Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Gloria Matemu amesema mpaka sasa Tanzania bado inauhitaji mkubwa wa vifaa tiba na vitendanishi ili kujihakikishia vinazalishwa nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waagizaji Dawa Tanzania (TAPI) Churchill Katwazwa amesema kuwa uwepo wa maonyesho yatawasaidia kugundua teknolojia mpya ya dawa na vifaa tiba.
Hata hivyo vyama mbalimbali vitashiriki kwenye maonyesho yao ni pamoja na Chama cha Wafamasia Tanzania,Chama cha Madaktari binwa wa upasuaji na Chama cha madaktari wanawake Tanzania.





Post a Comment