KAMPUNI YA ESSENTIAL LIMITED YADHAMILIA KUKUZA SEKTA KILIMO.



                                                
******
Timothy  Marko .

Katika kuhakikisha Sektaya kilimo inakuwa hapa nchini,Taasisi ya Essential Group Limited imewataka 
wakulima Mkoani Njombe wilaya Makete kuweza kuchangamkia fursa za kupata za kilimo kupitia taasisi hiyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Joel Kamoga juu yafursa mbalimbali zinazo tolewa na Kampuni ya Essential Group ambapo amesema kampuni hiyo imekuwa na uzoefu wa miaka 15 kwa kuagiza mizigo mbalimbali kutoka nje kiwemo zana zakilimo .

"Lengo letu nikuhakikisha Mkulima anakuza kilimo chake hasa mkulima wa Makete Mkoani Njombe".Alisema Joel Kamoga.

Kamoga,alisema sambamba na kujishugulisha nakuzaji wa sekta za kilimo pia kampuni yake imekuwa ikijishughulisha na utoaji mizigo ya ndani na nje ya nchi na kuwataka wananchi waweze kutumia kampuni hiyo katika uagizaji wa mizigo na kutuma Mizigo nje na ndani ya nchi. 

"Kwamiaka15 Nimekuwa nikijishughulisha na usafirishaji wa mizigo na uondoaji wa mizigo bandarini".Alisema Joel Kamoga.

Kamoga alisisitiza kuwa nimuhimu kwa watanzania kuzipa umuhimu kampuni za kizalendo katika kukuza uchumi nchini.

0/Post a Comment/Comments