Timothy Marko.
Chama cha watu wenye Ualbino(TAS)pamoja Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) vimelaani Vikali kitendo kilichofanywa na Klabu ya Simba siku ya simba Day Agosti 6 Mwaka huu kumtumia mtu Mwenye Ualbino mithili ya Mtu aliyekuwa hali ya nusu utupu na aliyevaa nepi yamkojo Jukwaani Mbele ya Hadhira ya maelfu katika uwanja wataifa.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa kituo Cha Haki za binadamu (LHRC) wakili Anna Henga amesema tukio hilo nimarudio ya tukio lililo fanywa Agosti8 Mwaka jana ,ambapo timu hiyo ilitumia jeneza na msalaba na kumnasibu mtu mwenye ualbino kama Msukule.
"Vitendo hivi vinatweza utu wawatu wenye ualbino nchini vinapelekea kuwa na mijadala mitandaoni na dhihaka kwa watu wenye ualbinokinyume na haki za binadamu"Alisema Wakili Anna Henga.
Wakili Henga alisema kuwa kwa miaka mingi jitihada kubwa zimekuwa zikifanyika katika utetezi kwa watu wenye ualbino kutokana nahistoria ya watu hao kupoteza maisha na idadi kubwa ya wahanga wa vitendo vya ukatili na unyanyapaa.
Alisema kuwa kwa Mujibu wa lbara ya 12(2)ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka1977 kila mtu anastahili heshima kutambuliwa na uthaminiwa utu wake.
"Ibara hii inaakisi ibara ya 8 ya Mkataba wa watu wenye ulemavu inayokomesha vitendo vya ukatili".AliongezaWakili Henga.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ualbino (TAS) Godson Moleli amesema kuwa ni Vyema taasisi zenyeushawishi kwenye Jamii kuepuka vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watu wenye Ualbino.
Alisema Nivyema watu wenye ualbino kukemea vikali vitendo hivi kwa Albino nikama watu wengine.
"Tunataka uongozi wa Simba uombe radhikwa watu Ualbino".Alisema Moleli.

Post a Comment