LESENI DARAJA C NA E ZA MADEREVA 8,237 ZAZUIWA NA POLISI




Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania, Ramadhani Ng’anzi  Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Ijumaa August 05 2023,  Makao makuu ya jeshi hilo. 




Waandishi wa habari na wapiga picha wa vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini wakimsikiliza Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania, Ramadhani Ng’anzi  mapema leo Ijumaa August 05 2023, Makao makuu ya jeshi hilo. 

(PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY) 
                            *******

Na Mwandishi wetu.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani  limezuia leseni  8,237 za Madereva  wa Madaraja C na E baada ya kubainika kukosa Sifa ya kuwa na madaraja hayo. 

Kuzuiliwa kwa Leseni hizo kunatokana na uhakiki uliofanywa na Jeshi hilo kuanzia Machi 1,2023, ambapo madaraja C na E  yako 72,560 nchi nzima na 8237 yakizuiliwa kwa kukosa Sifa ya kuwa na madaraja hayo huku jumla ya madaraja yote yakiwa 1725,373. 

Akizungumza mapema leo Ijumaa August 05 2023, Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania, Ramadhani Ng’anzi amesema kuwa kuzuiliwa kwa madaraja hayo kunatokana na sababu za Madereva hao kutosomea madaraja husika. 

Aidha amesema zoezi Hilo limetamatika Mwezi Julai 31,2023 huku zoezi likiwa endelevu kwa wale Madereva wenye sababu maalumu. 

Hata hivyo Kamanda Ng’anzi  amewataka wale wote wanaoamua kufanya mazoezi barabarani kutumia njia za watembea kwa miguu pia wakiona kuna umuhimu wa kutumia barabara Kuhakikisha wanachukua tahadhari kwa vijaketi au nguo zinazoakisi Manga. 

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limefanya uhakiki wa shule na vyuo vinavyotoa mafunzo ya udereva ambapo wamehakiki Shule na vyuo 297 na kubaini vyenye Sifa ni 134 huku 161 vikifungiwa kutoa mafunzo ya udereva kwa kuwa havikidhi Sifa na vigezo vinavyotakiwa.

0/Post a Comment/Comments