MAMA/BABA LISHE WAPEWA MITUNGI YA GESI BURE MACHINGA COMPLEX




Naibu Spika wa Bunge la Tanzania , na mbunge wa Jimbo la Ilala Azan Zungu akizungumza wakati wa utoaji wa mitungi ya gesi ya kupikia 40 kwa Mama na Baba lishe katika soko la Machinga Complex.


Mitungi ya gesi ya kupikia 40 kabla ya kugawiwa kwa Mama na Baba lishe katika soko la Machinga Complex.  



Mama na Baba lishe katika soko la Machinga Complex Wakikabidhiwa Mitungi ya Gesi. 
**********
(PICHA NA JAMES SALVATORY) 

NAIBU Spika wa Bunge la Tanzania , na mbunge wa Jimbo la Ilala Azan Zungu amegawa mitungi ya gesi ya kupikia 40 kwa mama na baba lishe katika soko la Machinga Complex.

Ugawaji wa mitungi hiyo ni sehemu ya mitungi 200 iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa masoko ya Machinga Complex, Karume, Ilala na Mchikichini.

Akizungumza wakati  zoezi Hilo LA ugawaji wa mitungi hiyo Zungu amesema kuwa upikiaji wa gesi unafaida nyingi ikiwemo kuokoa fedha na kuepukana na madhara ya moshi ambapo amedai kuwa mtu anayepikia kuni na mkaa kwa siku ni sawa na mtu anayevuta sigara 300.

Kwa upande wake Meneja wa somo la Machinga Complex Stella Mgumia amewahimza wafanyabishara wanafanya biashara ndogondogo katika maeneo yasio ruhusiwa kuondoka Mara moja na kwenda sehemu sahihi. 

Nao Mama lishe na Baba lishe mama na baba lishe katika soko la Machinga Complex wamesema Mitungi hiyo itaenda kuwasaidia katika shughuli zao za kila. 

 


0/Post a Comment/Comments