Timothy Mako
KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Sophia Mjema amewataka wanachama wa chama hicho kuweza kufahamu itikadi na ilani ya chama chama cha Mapinduzi sambamba na Misingi ya chama hicho.
Akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha wanachama wa chama hicho jijini Dar es Salaam Sophia Mjema amesema kuwa ni vyema wanachama cha Mapinduzi (CCM)wakafahamu wajibu wakuwa mwanachama wa chama cha Mapinduzi.
"Ukilisemea Vibaya jambo la chama chetu wenzako watalisema kwa Viongozi halafu badaye usije ukalaumu utakapochukuliwa hatua za kinidhamu,halafu ukajuta".Alisema Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Sophia Mjema.
Mjema alisema unapotaka kulisemea jambo lazima uwena ujuzi na hoja yakulisemea jambo hilo.
Alisema unaposema jambo lazima ujue Maadili hajalishi nikiongozi au mwanachama ndio uliseme jambo.
"Hapa hatuna Makundi hapa tuna chama cha Mapinduzi,Nilazima uyaseme Mazuri yaliyofanywa na Mwenyekiti".Alisisitiza Sophia Mjema.
Mjema alibainisha kwa wanachama wa chama hicho kuwa viongozi wa chama hicho ni sawa na wazazi hupaswi kuwa semea vibaya.
Aidha,Mjema aliongeza kuwa haipaswi kwa mwanachama wa chama hicho kuwa semea vibaya viongozi kwani viongozi wa chama hicho ni sawa na wazazi.
"Kazi yetu ni kumlinda kiongozi wetu,lazima useme Mazuri kwa mwenyekiti kuwa ametekeleza Miradi hii na uitaje" Alisisitiza Sophia Mjema

Post a Comment