MRAKIBU MWANDAMIZI MUGISHA ASISITIZA WANANCHI KUPELEKWA RAMANI ZA MAJENGO

Mrakibu Mwandamizi na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni ambao unahudumia Wilaya mbili za Kiserikali Kinondoni na Ubungo Elisa Mugisha wakati akizungumza na waandishi wa habari.
 .........................

NA MUSSA KHALID 

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni limewataka wananchi wanaojenga majengo katika mkoa huo kuhakikisha wanazipeleka ramani zao kwa jeshi hili ili kuepukana na changamoto wakati wa uokozi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mrakibu Mwandamizi na Kamanda wa Jeshi  la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni ambao unahudumia Wilaya mbili za Kiserikali Kinondoni na Ubungo Elisa Mugisha wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa ramani.

Mrakibu Mwandamizi Mugisha amesema kuwa ni muhimu ramani kupitishwa kwani kinga na tahadhari ya moto inaanzia katika usanifu wa jengo ili kunapotokea changamoto inayohitaji uokozi wanafanikisha kwa wakati.

‘Hiyo itasaidia kuangalia wakati wakutoka watu wengi watatokaje,milango imekaaje hivyo tunaendelea kuwasisitiza wananchi wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na Kinondoni wazilete ramani zao za majengo kwani kutofanya hivyo itakuwa wamevunja sheria”amesema Kamanda Mugisha

Aidha amesema kuwa Manispaa ya Ubungo hawana muamko wa kupeleka ramani hizo kama ilivyo kwa Manispaa ya Kinondoni hiyo amewataka kabla ya hatua kuchukuliwa ni vyema wakatekeleza hilo.

Katika hatua nyingine Kamanda Mugisha ameisisitiza jamii kuendelea kutoa taarifa pindi wanapopata dharura yeyote ya maokozi kupitia namba 114 ili waweze kupata msaada wa haraka na kuepusha lawama ya kuchelewa kufika.

Pia Kamanda Mugisha amesema wataendelea kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kupeleka taarifa za maeneo yao kabla ya kuanza ujenzi.

0/Post a Comment/Comments