MSAMA:TUSIMDHIHAKI RAIS





********

 Mfanyabiashara maarufu ambae pia Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amewakemea baadhi ya Watu ambao kwa makusudi wanatumia mitandao ya Kijamii Kumdhihaki Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Maslahi yao Binafsi, 

Msama amekieleza Kitendo hicho kuwa sio cha Kiungwana na sio Mila na Desturi ya Watanzania kwa Sababu kinalenga kuligawa Taifa .

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Msama ameomba Mamlaka zinazohusika  kushughulika na wote wanaofanya vitendo vya kiutovu wa Nidhamu  kwa Rais wa  Tanzania.

"Kwa Siku za hivi Karibuni kumeibuka Kikundi cha watu wachache ambao kutokana na Nia yao Ovu dhidi ya Taifa la Tanzania na Kwa Maslahi yao Binafsi wamekuwa wakitumiw Mitandao ya Kijamii kubeza kazi nzuri inayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Watanzania wote, binafsi Sifurahishwi na Maneno ya Kejeli yanayoelekezwa kwa Kiongozi mkuu wa Nchi, Hivyo ninaomba mamlaka zinazohusika kuanza kuchukua hatua za Kisheria kwa Wanaotumia Mitandao ya Kijamii kumtusi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan" amesema Alex Msama.

Aidha ameongeza kuwa Suala la kuendelea Kufumbia macho Vitendo hivyo, linaweza kuathiri pakubwa Ustawi wa Taifa la Tanzania ambayo inasifika kuwa Kisiwa cha Amani na Taifa linalovutia kwenye Suala zima la Uwekezaji.

"Tanzania kama nchi imekuwa ikisifika Ulimwenguni kama Kisiwa cha Amani na Eneo muhimu lenye mazingira mazuri kwa ajili ya Kuvutia Wawekezaji, kwa hiyo tusiache watu wachache wakaipaka matope nchi yetu hatua ambayo itafanya wawekezaji kukimbia.

0/Post a Comment/Comments