NHC KUWAPELEKA WADAIWA SUGU KWENYE MAMLAKA ZA MIKOPO ILI KUSITISHA MIKOPO YAO



Meneja Habari na Mahusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa nchini(NHC) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.




........................

Timothy Marko

SHIRIKA la Nyumba la Taifa nchini(NHC) limewataka wapangaji wa Nyumba za NHC kulipa malimbikizo ya madeni sambamba na kodi kwa wateja wanaodaiwa kupitia shirika hilo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja Habari na Mahusiano wa Shirika hilo Muungano Saguya amesema hadi kufikia mwaka huu shilika hilo limekuwa likidai madeni ya Awali ya shilingi bilioni 28 lakini Baada ya kutumia mbinu mbali ikiwemo funguo janja wameweza kukusanya shilingi bilioni 5 kutoka kwa wadaiwa sugu.

"Kwa wapangaji waliopo kwenye Nyumba ambao watashindwa kulipa kodikwakipindi cha mwezi mmoja Shirika litavunja mkataba nakuwaondoa kwa mujibu wa sheria"Meneja Saguya.

Saguya alisema kuwa kwa wapangaji ambao wamepewa notisi za kulipa kodi wanayo daiwa utekelezaji wa notisi hizo utaendelea.

Aliongeza kuwa nivyema wapangaji wa nyumba hizo kutekeleza wajibu wao kama ilivyo elekeza ilikuepukana na usumbufu.

"Shirika limeanzisha makubaliano na Credit Info bureu ilikupeleka majina ya wadaiwa sugu ili wasiweze kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha"Alisisitiza Saguya.

0/Post a Comment/Comments