WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, ameishauri Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), iangalie namna ya kufadhili Tafiti zenye kuweza kupeleka Teknolojia kwa Wakulima ambao bado wanahangaika na jinsi ya kuongeza thamani ikiwemo kupata soko sahihi.
Pinda amesema hayo leo alipotembea Banda la COSTECH katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale vilivyopo jijini Mbeya.
Ukiacha hayo Pinda ameshauri COSTECH kufikiria kuanzisha wiki ya matokeo ya Tafiti zenye tija kwenye Jamii kwa kushirikiana na Taasisi za Utafiti na Vyuo Vikuu, huku akiipongeza serikali kupitia COSTECH kwa kuendelea kufadhili Taasisi za Maendeleo ya Utafiti TARI Tengeru kutokana na mradi wa uzalishaji wa migomba maabara kwa njia ya chupa ( Tissue Culture).
Mtafiti kutoka TARI Tengeru Bw. Benjamin Bitalibube amesema mpaka sasa imeshapeleka Miche ya migomba zaidi ya elfu 30 kwa wananchi wa mikoa mitano ya Mbeya, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro na Kagera, huku wananchi wakipata Elimu juu ya Kilimo cha migomba.
Kwa upande wa Teknolojia ya sumu ya nyuki Mhe. Pinda amesema Uvunaji wa maziwa ya nyuki usichanganywe na asali na virutubisho vya maziwa ya nyuki amesisitiza vipimwe.





Post a Comment