Timothy Marko.
Jeshi la polisi kanda maalum jijini Dar es salaam lina Mshikilia Selemani Hagai (18) Mkazi wa kigamboni kwa tuhuma za kutoa lugha Chafu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutumia video aliyoituma kwenye mtandao wa tiktalk.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kamishina wa kanda maalum Murilo Jumanne Murilo amesema kuwa mtuhumiwa huyo Julai 29 mwaka huu alijirekodi na kutuma video yenye Maudhui ya kashfa kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassani nakurusha katika mtandao wa tiktalk.
Katika hatua nyingine Kamishina wa kanda hiyo Murilo Jumanne Murilo amesema Jeshi la polisi kanda ya Dar es salaam lina washikilia watu saba kwa kusababisha kifo cha Khadija Hamisi Mkazi wa vingunguti.
Alisema watu wanne wamelazwa katika hospitali ya Amana ya jijini Dar es salaam kwa matibabu.
"Wito wangu wale wote waliohusika na matendo haya watafikishwa Mahakamani".Aliongeza CP Murilo.

Post a Comment