POLISI YAWASHIKILIA ASKARI TFS KWA TUHUMA ZA KUJERUHI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI

........................

Timothy Marko 

Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia Askari polisi(6) wakiwemo Askari wa kampuni ya ulinzi pasco Lmited ,Maafisa wa Misitu (TFS)wawili  kwa kusababisha Majeraha navifo vya watu wawili .

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kamishina wa polisiwa kanda Maalum ya Dar es Salaam CP Murilo Jumanne Murilo amesema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 28 Mwaka huu saa tatu katika Maeneo ya  kiluvya, ubungo jijini Dar es Salaam.

"Wakiwa katika majukumu yao katika  kuhakikisha Mazao ya Misitu yanalindwa ,Maafisa hao walikutana na nawatu 30na kuwataka wasimame walikaidi Amri hiyo ndipo Maafisa  hao waliamua kufyatua Risasi hewani nakujeruhi watu wawili na kupoteza maisha"Alisema Kamishina Murilo Jumanne Murilo

Kamishina Murilo alisema Askari hao wanashikiliwa na Jeshi la polisi na kukamatwa kwa matumizi ya nguvu ya Silaha kupita kiasi na kuhojiwa.

Aliongeza kuwa Jeshi hilohalitasita  kuwachulia hatua waliohusika natukio hilo na kubainisha mili ya watuhao waliojeruhiwa na wengine kufariki dunia imehifadhiwa  katika hospitali ya Mloganzila kwa uchunguzi zaidi.

 

0/Post a Comment/Comments