PRF MBARAWA:BARABARA YA MWENDOKASI GMBOTO IKAMILIKE KWA WAKATI



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Mohamed Besta na Mkandarasi SINOHYDRO Corporation Ltd alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Usafiri wa Haraka wa Mabasi BRT III jiji la Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Usafiri wa Haraka wa Mabasi BRT III kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongolamboto KM 23.3 jijini Dar es Salaam.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Mohamed Besta akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Usafiri wa Haraka wa Mabasi BRT III kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongolamboto KM 23.3, inayojengwa na Mkandarasi SINOHYDRO Corporation Ltd leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Tawala Wilaya ya Ilala, Charangwa Selemani akizungumza juu ya maendeleo ya mradi huo na namna utaenda kuwasaidia wananchi wa wilaya hiyo. 



Muonekano wa Ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo haraka kwa awamu ya tatu BRT3 kutoka katikati ya Jiji hadi Gongo la Mboto ukiendelea kujengwa 

Muonekano wa Ujenzi wa  kituo cha  Mabasi yaendayo haraka kwa awamu ya tatu BRT3 kutoka katikati ya Jiji hadi Gongo la Mboto kikiendelea kujengwa. 



Sehemu ya kutengenezea Makalavati na baadhi ya vifaa vitavyotumika kujenga Barabara ya Mabasi yaendayo haraka kwa awamu ya tatu BRT3 kutoka katikati ya Jiji hadi Gongo la Mboto. 

               (PICHA NA JAMES SALVATORY) 

                              ******

Na Mwandishi With. 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ameagiza, Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kuhakikisha mradi wa ujenzi Barabara ya Mabasi yaendayo haraka awamu ya tatu BRT3  kutoka katikati ya Jiji hadi Gongo la Mboto unatekelezwa kwa wakati na viwango vinavyotakiwa. 


Amesema hayo baada ya kufanya ziara katika mradi huo wenye urefu wa Kilomita 23.3 pamoja na Vituo mbalimbali vya abiria ambapo amempongeza Mkandarasi anayejenga kwa kasi anayoenda nayo licha ya kuchelewa kidogo.

Aidha Profesa Mbawara amesema kuwa mkandarasi kaajili vijana 94 Kwa ajili ya kusaidia kwenye ujenzi huo wakifanya kazi usiku na mchana ili kurahisisha kazi na kumaliza kazi Kwa wakati.


Msimamizi wa Mradi huo Mhandisi Frank Mbilinyi amesema mradi umefikia asilimia 12 na kwamba shughuli za Ujenzi zinaendelea kufanyika mchana na usiku huku akiahidi utakamilika kwa muda uliopangwa kutokana na umuhimu wa Barabara hiyo kwa Wananchi.

“Tunatambua umuhimu mkubwa wa barabara hii tunafanya kazi usiku na mchana ili kuikamilisha kwa wakati ili kuwaondolea usumbufu wananchi”amesema Mbilinyi
Aidha Mbilinyi amesema mradi wa mbagala umechelewa Kwa asilimia mbili kutokana na sababu mbalimbali lakini unatarajiwa kukamilika mwezi wa wa kumi.

Amesema mpaka Sasa ni marekebisho madogo yaliyobaki ili kukabidhiwa ikiwemo taa na miundombinu ya vituo.

“Huu mradi umechelewa kweli Kwa asilimia mbili lakini mpaka kufikia mwezi wa kumi tutakua tumeukamilisha na kukabidhi Kwa ajili ya kuanza kazi sehemu zilizobaki ni ndogo ndogo.

 Ameongeza Mbilinyi
Akizungumza katika ziara hiyo Katibu tawala wa Wilaya ya Temeke Nicodemas Tambo na Katibu tawala Charangwa Seleman wamesema Barabara hiyo inawatumiaji wengi hivyo wamesisitiza ikamilike Kwa wakati ili kuwapunguzia Wananchi kero.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Ilala, Charangwa Seleman alisema mradi huo ni muhimu kwa wakati wa Wilaya ya Ilala, hivyo alumshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuleta mradi huo wa BRT 3 na kuwaomba wakandarasi kuongeza spidi ujenzi ili iweze kuwahudumia wananchi.

Katibu Tawala Wilaya ya  Temeke Nicodemus Tambo, alumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za mradi huo kwani nimradi muhimu kwa wananchi na wageni kutoka nje ya nchi na uchumi wa Taifa kwa ujumla. 

Hii barabara inategemewa sana na Wananchi Kwa shughuli zao za kiuchumi na kijamii hivyo mradi huu unapaswa ukamilike Kwa wakati ili kuwapunguzia wananchi kero wanayokutana nayo Sasa”amesema Charangwa.

Hadi kukamilika kwa mradi huo unatarajia kugharimu shilingi bilioni 231.



0/Post a Comment/Comments