RC MTAKA AIPONGEZA COSTECH KWA KUBEBA DHANA YA KILIMO BIASHARA

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka akitembelea Banda la COSTECH katika Maonesho ya kitaifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea jijini Mbeya.

....,................

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka ameipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kutokana na kubeba dhana ya Kilimo Biashara ikiwemo kuwa taasisi inayosaidia watafiti na wabunifu.

Mtaka amesema hayo alipotembelea Banda la COSTECH katika Maonesho ya kitaifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea jijini Mbeya.

Mbali na hayo Mtaka ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuuwisha COSTECH na kuendeleza Tafiti na Bunifu zinazofanywa na Vijana katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Vilevile amesema kwenye mageuzi ambayo Serikali inafanya sasa hususani maamuzi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kutamani nchi iwe inalisha bara la Afrika kwa kuwaendeleza watafiti na wabunifu wakazalisha bidhaa zenye tija zitakazoinua Taifa letu kiuchumi.

Mtaka ameishauri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Kilimo kushirikiana ili kuendeleza Teknolojia zitakazowezesha kufanya vizuri zaidi.

Hata hivyo ameipongeza COSTECH kwa kuendelea na kukuza Tafiti na Bunifu ikiwemo kuwashauri washiriki na viongozi kutembelea Banda la COSTECH.

Mtaka amewaalika kushiriki Maonesho ya Viwanda vidogovidogo Sido yatakayofanyika mkoani Njombe ambapo COSTECH watakuwa wadau wakubwa na kusaidia kuwaalika vijana kushiriki Maonesho hayo.

0/Post a Comment/Comments