SERIKALI KUJENGA MASOKO YAKISASA CHANIKA NA G/MBOTO.



******
 Timothy Marko.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka Wafanyabiashara wadogowadogo(WAMACHINGA)amesema Serikali ya mkoa wa Dar es salaam inayompango kujenga Masoko manne katika Maeneo ya Ilala,Gongolambo na aChanika ilikuboresha Huduma za wafanyabiashara wadogowadogo .

Akizungumza katika Mkutano wa Hadhara na Wamachinga katika viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar es Salaam Albert Chalamila amesema Serikali inayompango wakuwapatia mavazi maalum kwa madereva wa bodaboda ili kuweza kutambulika.

"Tutahakikisha Dereva wa boda boda wanatambulika kwa mavazi yao".Alisema Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila.

Chalamila aliongezakuwa serikali ipobega kwa bega na wamachinga.

Naye Mwenyekiti wafanyabiashara wadogowadogo(WAMACHINGA) Yusufu Namoto amesema Jumuhiya hiyo inamuunga Mkono RaisDk Samia suluhu Hassani katika kuboresha sekta ya Elimu na uboreshwaji wa sekta ya Afya.

"Tunamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta Anga na utalii".Alisema Mwenyekiti yussufu Namoto.

0/Post a Comment/Comments