SIMBA KUHIFADHI NYARAKA ZAKE MAKUMBUSHO YA TAIFA.




*****"
Timothy Marko

Klabu ya Mpira ya Simba imesema itaendelea kuweka kumbukumbu za taarifa pamoja na Vielelezo vya klabu hiyo kwenye Makao Makuu Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam .

Akizungumza nawaandishi wa Habari kwenye Ofisi za makumbusho ya taifa Afisa Habari wa klabu hiyo Ahmed Ali amesema Vielelezo vya timu hiyo na Historia ya timu hiyo ikiwemo kibegi cha Simba kuanzia kuanzishwa kwa timu hiyo 1936 na siku za mbeleni historia hiyo itapatikana kwenye Makumbusho ya taifa.

"Kuanzia Sasa historia ya timu ya Simba na Vielelezo vyake ikiwemo kibegi cha Simba kitapatikana katika makumbusho ya taifa".Alisema Msemaji wa Simba Ahmed Ally.

Ahmed Ally alisisitiza historia ya Mwaka 1936 ya Tangu  kuanzishwa kwa timu ya Simba utapatikana Kwenye Makumbusho ya taifa.

Aliongeza katika kuelekea Maadhimisho ya Simba Day Jumapili  wanamtarajia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kuwa Mgeni Rasmi wa tukio la Simba Day.

0/Post a Comment/Comments