STAMICO YAONGEZA UKUSANYAJI MAPATO ZAIDI YA MARA 60




Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse akizungumza katika Mkutano uliojumuisha Ofisi ya Msajili wa Hazina, STAMICO, na wahariri wa Vyombo vya habari, uliofanyika leo Agosti 28,2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.




Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, akizungumza alipokuwa akitoa neno kwa niaba ya Wahariri waliohudhuria katika mkutano huo, uliofanyika leo Agosti 28, 2023 Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.


wahariri na Waandishi wa Vyombo vya habari Mbalimbali wakifuatilia wasilisho la Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse katika Mkutano wa Taasisi hiyo na Wahariri wa Vyombo vya habari, kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
******
 Na Mwandishi Wetu
                   
Shirika la madini la Taifa (STAMICO) limesema limefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa Mapato ya ndani kutoka Shilingi Bilioni1.3 kwa Mwaka 2018/19 hadi Shilingi Bilioni 61.1 kwa mwaka 2022/23 ambalo ni ongezeko la asilimia zaidi ya 4425

Akizungumza Mapema Leo jijini Dar es salaam na Jukwaa LA wa Hariri (TEF) kuhusu utekelezaji wa shughuli za shirika hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse  amesema tangu kuanzishwa kwa shirika Hilo mwaka 1972, halikuwahi kupeleka kitu chochote serikalini ambapo kwa sasa tangu wapate mafanikio hayo limefanikiwa kulipa Gawio serikalini Jumla ya Shilingi Bilioni 8.

Mkurugenzi huyo amesema  shirika hilo lilikuwa linakwenda kufutwa lakini mikakati ya ndani na kuwezeshwa na Serikali ikiwemo kubadili muundo wa shirika, ndio sababu iliyolifanya kufika hapo lilipo.

Katika hatua nyingine Dkt Mwasse amebainisha mikakati mbalimbali ya shirika hilo ikiwemo kuondoa kabisa utegemezi wa mishahara kutoka serikalini kuanzia mwaka wa fedha 2024/25.

Pia Mkurugenzi Mkuu wa Stamico, amesema wanakusudia kuanzisha Benki ya wachimbaji wadogo ikilenga kuwaondokana kero ya kutokopesheka kwenye Mabenki na itawasaidia kukuza mitaji na uchumi wao.

Katika kuwaendeleza wachimbaji wadogo, Dokta Mwasse, amesema Stamico imenunua mitambo mitano ya kufanya uchorongaji na kwamba mitambo hiyo inatarajiwa kufika nchini mwezi Septemba mwaka huu.

Kwa upande Wake MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),Deodatius Balile  ameishauri STAMICO kujali maslahi ya wafanyakazi wao huku akiomba ujuzi walio nao kuhamishia katika taasisi zingine za Serikali.





0/Post a Comment/Comments