TMA YATABIRI UWEPO WA MVUA ZA JUU YA WASTANI HADI WASTANI KATIKA MAENEO MENGI YA NCHI.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi  wakati wa mkutano na vyombo vya habari kuhusiana na mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli (Oktoba hadi Disemba 2023) Dkt. Ladislaus Chang’a akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusiana na mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli (Oktoba hadi Disemba mwaka huu.

........................ 

NA MUSSA KHALID

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya Pwani ya Kaskazini na Ukanda wa Ziwa Victoria katika msimu wa mvua za Vuli, 2023.

Mamlaka hiyo imetaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, kusini mwa mkoa wa Simiyu, kaskazini mwa mkoa wa Kigoma,Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikiwemo visiwa vya Mafia), kaskazini mwa mkoa wa Morogoro na pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba  huku mikoa ya Mara, kaskazini mwa mkoa wa Simiyu, Arusha, Manyara na Kilimanjaro yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi Dkt. Ladislaus Chang’a  wakati wa mkutano na vyombo vya habari kuhusiana na mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli (Oktoba hadi Disemba 2023),ambapo amesema kutokana na uwepo wa El-Niño, vipindi vifupi vya mvua vinatarajiwa kwa mwezi Septemba, 2023 katika baadhi ya maeneo nchini, hata hivyo, mvua za Vuli, 2023 zinatarajiwa kuanza rasmi mwezi Oktoba, 2023 katika maeneo mengi.

“Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2023 katika maeneo ya magharibi mwa Ziwa Victoria na kusambaa katika maeneo mengine mwezi Oktoba, 2023.

Kwa kawaida mvua za Vuli huisha mwezi Disemba, hata hivyo msimu huu mvua za nje ya msimu zinatarajiwa kuendelea mwezi Januari, 2024. Ongezeko la mvua linatarajiwa mwezi Disemba, 2023”. Alisema Dkt. Chang’a 

Dkt. Chang’a atoa wito kwa wananchi kufuatilia taarifa za utabiri wa saa24, siku 10, mwezi natahadhari zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ikizingatiwa kuwa mwelekeo wa mvua uliotolewa ni kipindi cha msimu wa miezi mitatu, hivyo viashairia vinavyochangia mwenendo wa mifumo ya mvua na mabadaliko ya muda mfupi utazingatiwa katika uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na mfupi. 

Aidha Dkt Chang’a ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wadau wa sekta kushirikiana na wataalamu mbalimbali ikiwemo wa hali ya hewa ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.

Awali Mtaalamu na mchambuzi kutoka TMA Rose Sinyagwa akitoa mrejesho wa utabiri wa msimu wa mvua za masika tathimini inaonyesha mvua hizo zilinyesha kwa wastani katika maeneo mengi yanayopata mvua za masika.

Hata hivyo Mamlaka hiyo imewashauri watumiaji wote wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na wakulima,wafugaji,Mamlaka za wanyamapori,wasafirishaji,Mamlaka za maji na Afya kuhakikisha wanaendelea kuafuta,kupata na kuzingatia ushauri wa wataalamu katika sekta husika.

0/Post a Comment/Comments