Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a (katikati),Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri (TMA( Dkt Hamza Kabelwa (Kulia) Pamoja na Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA Monica Mutoni (kushoto) wakiongoza warsha ya wanahabari ambayo imefanyika Leo Kibaha Mkoani Pwani.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a, wakati akifungua warsha ya wanahabari ambayo imefanyika Leo Kibaha Mkoani Pwani
Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA Monica Mutoni akizungumza katika warsha ya wanahabari ambayo imefanyika Leo Kibaha Mkoani Pwani.
Baadhi ya wanahabari kutokea katika Vyombo mbalimbali vya habari nchini wakisikiliza kwa makini Mafunzo wanayopatiwa katika warsha ya wanahabari ambayo imefanyika Leo Kibaha Mkoani Pwani.
Picha ya pamoja Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a, akiwa na washiriki wa warsha ya wanahabari ambayo imefanyika Leo Kibaha Mkoani Pwani.
.........................
NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania -TMA imeendelea kuwasisitiza wanahabari nchini kuendelea kuwa mabalozi wa kusambaza Taarifa za Hali ya Hewa zinazotolewa na Mamlaka hiyo Ili wananchi waweze kuzipata Kwa usahihi.
Kauli hiyo imetolewa Mkoani Pwani na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a, wakati akifungua warsha ya wanahabari yenye lengo la kuwajengea uwezo wa namna ya kuandika na kuripoti taarifa za Hali ya Hewa.
Amesema ufanyaji wa Warsh umekuwa ni muendelezo wa mara kwa mara wa kukutana na wanahabari na kuwajengea uwezo wa namna ya kuzifikisha taarifa za Hali ya Hewa Kwa jamii.
" Taarifa zikiwafikia walengwa kwa usahihi zinaweza kuwaepusha wananchi na majanga hivyo Mamlaka itaendelea kujitahidi kutoa taarifa zake Kwa wakati"amesema Dkt Chang'a
Amesema kuwa upatikanaji wa taarifa sahihi za hali ya hewa ni muhimu kwa sababu zina mchango mkubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, nishati, maji.
Aidha, Dkt. Chang’a amesema kuwa Serikali imeendelea kuijengea uwezo TMA na kuifanya iendelee kuimnarisha huduma ikiwemo utoaji wa taarifa hizo kuwafikia watumiaji kwa wakati na kufanya maamuzi sahihi kwa wakati muafaka.
Katika hatua nyingine Dkt Chang'a Dkt. Chang’a amewaeleza wanahabari katika warsha hiyo kuwa msimu unaokuja wa Oktoba hadi Disemba 2023 utachagizwa na uwepo wa El Nino ambayo ni hali ya kuongezeka kwa joto la uso wa bahari kwa eneo la kitropiki la kati ya Bahari ya Pasifiki, hali ambayo husababisha kuongezeka kwa viwango vya mvua na joto kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri (TMA( Dkt Hamza Kabelwa amewasisitiza waandishi wa habari kutoyumbishwa na Taasisi za Nje bali wasubirie taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa Matukio.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA Monica Mutoni ameeleza uhusiano uliopo baina ya Mamlaka hiyo na vyombo vya habari kuwa ni mkubwa jambo linalosaidia taariza zao kuwafikia watanzania kwa wakati.





Post a Comment