Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi
Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania (Commandant TPS- Moshi) SACP-Ramadhani Mungi amewakumbusha na kuwataka wachezaji wa Timu ya Polisi Tanzania kuweka Juhudi zaidi katika Michezo yao ili kuiwezesha timu hiyo kurejea ligi kuu ya Tanzania Msimu ujao.
Kauli hiyo ameotoa Leo agosti 09,2023 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Shule ya Polisi Tanzania ambapo SACP Ramadhan Mungi amewakumbusha wachezaji hao kuwa bado Jeshi hilo lina imani kubwa na timu hiyo uku akiwataka wachezaji hao kuweka juhudi na jitihada ili kukamilisha ndoto ya kutwa ubingwa wa ligi iyo pindi watakapo rejea.
Ameongeza kuwa yeye aliwahi kucheza mpira wa Miguu na mwaka 1998 na alicheza mpira kwa mafanikio makubwa ambapo amewataka kuonyesha kiwango kwa daraja hilo walilopo kwa sasa baada ya kushuka kutoka ligi Kuu.
Amewakumbusha kuwa mpira ni kazi ambayo inataka nidhamu na kuonyesha ushirikino (team work) ili kufikia malengo ambayo mashabiki na Timu hiyo wanatani kuyaona.
Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania ameahidi kutoa ushirikiano,pamoja na maafisa kutoka Shule hiyo.


Post a Comment