Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile akizungumza na kutoa shukurani sake kwa. Uongozi wa PSSSF mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam Leo.
Sabato Kosuri Afisa Uhusiano na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina akifafanua baadhi ya mambo muhimu katika kikao hicho.
Baadhi ya wahariri wa Vyombo vya habari wakifuatilia Wasilisho la Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF Hosea Kashimba, wakati wa Mkutano wa Ofisi ya Msajili wa Hazina,
******
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF),unaendelea na uwekezaji ili kutoa huduma zitakazoondoa kabisa changamoto katika utoaji huduma kwa wanaufaika wa Mfuko huo.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Dk Hoseah Kashimba amesema kwa kipindi cha miaka mitano ya mfuko huo kwa kiwango kikubwa wameshughulikia changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili Wastaafu,
"Tumefanikiwa katika kulipa bila kukosa na kwa wakati pensheni ya kila mwezi, Wastani wa shilingi bilioni 67 hulipwa kila ifikapo tarehe 25 ya mwezi husika, hili ni ongezeko la asilimia 100 ukilinganisha na kiasi cha shilingi bilioni 34 zilizokuwa zikitolewa hapo awali kila mwezi." amesema
Aidha ameongeza kuwa thamani ya mfuko huo imeongezeka kwa asilimia 27.76 kutoka shilingi Trilioni 5.83 hadi trilioni 8.07 na kupunguza gharama za uendeshaji.






Post a Comment