WAZIRI NDUMBALO AWAKUTANISHA MAWAZIRI WASTAAFU WA SHERIA KUJADILI MCHAKATO WA KATIBA MPYA.


...........................

Timothy Marko .

Kikao cha Mawaziri wa Sheria na Wanasheria wakuu wa staafu na waliopo madarakani wamekutana leo jijini Dar es salaam kujadili mchakato wa katiba mpya pendekezwa ambapo mchakato wake ulianza 2014.

Akizungumza katika kikao hicho kilicho wakutanisha Mawaziri wa sheria na wanasheria wastaafu mapema leo,jijini Dar es salaam Waziri wa Katiba na Sheria Dk .Damas Ndumbalo amesema kuwa lengo lakikao hicho kujenga Uelewa na kutoa Elimu juu ya Mwenendo wa Mchakatokatiba mpya.
"Zaidi ya Asilimia 50 ya Watanzania hawafahamu katiba ,kwahiyo kuna hatari yakuingizwa kwa mambo yasiyo ya kikatiba"Alisema Waziri wa katiba na Sheria Dk Damas Ndumbalo.

Dk Ndubalo alisema kuwa Majukumu ya wizara yake anayoiongoza nikuratibu mchakato wa katiba ya mwaka 1977.

Alisema hapo Awali Tume ili kamilisha Rasmu ya katiba na kuundwa Bunge la katiba ambapo mchakato wake ùlikoma mara baadaa ya wajumbe wa bunge hilo kususia Vikao.

"Kupitia kikao hiki tutapata maoni yenu kwa upande wa Zanzibar na Tanzania bara" .Aliongeza Waziri wa Katiba nasheria Dk Damas Ndumbalo.

0/Post a Comment/Comments