AFRIKA KUJADILI NAMNA YA KUPAMBANA HOMA YA INI.


......................

Timothy Marko

ZAIDI ya Nchi 43 barani Afrika zimekutana jijini Dar es Salaam katika kujadili namna ya kudhibiti ugonjwa Ini .

Akizungumza katika Mkutano wa kujadili namna kudhibiti ugonjwa huo wa ini Barani Afrika (Conference on Liver Disease in Africa) jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa taasisi ya Jakaya kikwete Health instute Profesa Mohamed Janabi amesema kuwa lengo la Mkutano huo nikujadili namna ya kufanya upasuaji wa ugonjwa huo ilikupunguza Gharama za matibabu ya ugonjwa huo.

"Ugonjwa huu waHoma ya ini unawaathiri sana watu wanaotumia madawa ya kulevya,Watu wenye Maambukizi ya HIV".Alisema Profesa Mohamed   Janabi.

Profesa Janabialisema Mkutano huo unaowakutanisha watalamu wa sekta ya Afya wa upasuaji wakutoka nchi 43 ikijumuisha nchi za Afrika kusini ,Misri,Tanzania ukiwa na Agenda ya namna yakufanya Matibabu ya Homa ya ini kwanjia ya upasuaji ilikuweza kupunguza Gharama za Matibabu za ugonjwa huo.

Alisema katika Ajenda za mkutano huo nikuangalia namna ya uwekezaji wa miundombinu ya sekta  ya Afya ilikuweza kutokomeza ugonjwa huo.

"Homa ya Ini nikati ya vyanzo vya Magonjwa namba nne vinavyo sababisha Vifo nchini".Aliongeza Profesa Mohamed Janabi.

Aliongeza kuwa lengo la serikali nikuhakikisha Chanjo ya ugonjwa huo inapatikana.

Naye Mhadhiri wa Chuo cha Misri AinShams University Profesa Manel El  Sayed amesema kuwa watu 100 wanne wana maambukizi wa ugonjwa ini.

Alisema lengo la Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la WHO nikuhakikisha Wahanga wa ugonjwa huo wanapata Chanjo.

"Homa ya ini inachangiwa na Ngono Zembe,Vitu vya Ncha kali "Alisema Manel El Sayed.

0/Post a Comment/Comments