AICC, JNICC VYAWATAKA WADAIWA KULIPA MADENI YAO


Mkurugenzi mtendaji wa AICC na JNICC Ephraim Mafuru akizungumza katika mkutano na wahariri na waandishi wa habari kuelezea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na vituo hivyo, mkutano uliofanyika Jinini Dar es Salam.




                      ******

Vituo vya mikutano vya kimataifa Arusha international conference center (AICC) na Julius   Nyerere International Conference Center (JNICC ) vimewataka  wateja wao ikiwemo baadhi ya taasisi mbalimbali za serikali kulipa madeni yao kwa wakati ili kuwezesha vituo hivyo kuendelea kujiendesha kupitia diplomasia ya mikutano mbalimbali inayochangia ukuaji wa pato la Taifa.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi mtendaji wa AICC na JNICC Ephraim Mafuru  katika mkutano na wahariri na waandishi wa habari kuelezea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na vituo hivyo, mkutano uliofanyika Jinini Dar es Salam.

Amesema zipo baadhi ya taasisi zimekuwa zikilimbikiza madeni yao ambapo hadi sasa vituo hivyo vinadai zaidi ya shilingi Bilioni 7.4.

Akizungumzia ukuaji wa vituo hivyo vya mikutano kwa miaka mitano ijayo MAFURU amesema kwa sasa wameendelea kufanya vizuri katika vituo vyote viwili na wamejipanga kujenga kituo kingine kikubwa zaidi na cha kisasa cha mikutano Mount Kilimanjaro International Conference Center (KICC) kitakachokuwa na uwezo wa kubeba watu zaidi ya 3000 ambacho kitachangia zaidi katika shughuli za utalii za kuongeza fedha za kigeni.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri (TEF) Deudatus Balile mjumbe kutoka jukwaa hilo Jane Mihanji amepongeza uwekezaji wa kidiplomasia wa mikutano unaofanywa na JNICC na AICC na kuwashauri kufanyia kazi yote waliyoshauriwa na jukwaa hilo ili kuendeleza utekelezaji ulio na maslahi kwa taifa na wananchi kwa ujumla.

0/Post a Comment/Comments