Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki nchini Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare akizungumza katika warsha ya kwanza kati ya tano zenye nia ya kutoa elimu ya ufahamu wa hakimiliki ambayo imeratibiwa na Mtandao wa Sekta Bunifu nchini Tanzania ikiwakutanisha wadau mbalimbali ambayo imefanyika jijini Dar es salaam.
Inocent Nganyagwa maarufu Ras Inno ni Mjumbe wa Bodi,Mwanzilishi na Katibu wa Mtandao wa Sekta Bunifu nchini Tanzania akizungumza katika warsha ya kwanza kati ya tano zenye nia ya kutoa elimu ya ufahamu wa hakimiliki ambayo imeratibiwa na Mtandao wa Sekta Bunifu nchini Tanzania ikiwakutanisha wadau mbalimbali ambayo imefanyika jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali katika warsha ya kwanza kati ya tano zenye nia ya kutoa elimu ya ufahamu wa hakimiliki ambayo imeratibiwa na Mtandao wa Sekta Bunifu nchini Tanzania ikiwakutanisha wadau mbalimbali ambayo imefanyika jijini Dar es salaam.
Katibu wa Wasanii wa Muziki Bongofleva Anselm Ngaiza au Soggy Doggy akizungumza katika warsha ya kwanza kati ya tano zenye nia ya kutoa elimu ya ufahamu wa hakimiliki ambayo imeratibiwa na Mtandao wa Sekta Bunifu nchini Tanzania ikiwakutanisha wadau mbalimbali ambayo imefanyika jijini Dar es salaam.
....................
NA MUSSA KHALID
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki nchini Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare amesema serikali imeanza mchakato wa kuwaruhusu wasanii na makampuni mbalimbali kusimamia masuala ya ukusanyaji wa mirabaha ili
Sinare amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye warsha ya kwanza kati ya tano zenye nia ya kutoa elimu ya ufahamu wa hakimiliki ambayo imeratibiwa na Mtandao wa Sekta Bunifu nchini Tanzania ikiwakutanisha wadau mbalimbali.
Aidha amesema kwa sasa sheria imefungua milango kwa wadau mbalimbali kuanzisha usimamizi wa masuala ya muziki kwenye upande wa ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha.
"Sheria imeruhusu uanzishwaji wa makampuni na wadau wenyewe kusimamia mambo yao kwa ajili ya kusimamia Masuala ya Muziki Kwenye Upande wa ukusanyaji na kusimamia mirabaha"amesema Sinare
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtandao wa Sekta Bunifu nchini Tanzania Robert Mwampembwa amesema kuwa baada ya sheria kubadilika hapakuwa na mafunzo na elimu kwa wabunifu jambo ambalo limewakosesha kipato.
Amesema baada ya Mwaka Jana sheria kubadilika ikiruhusu wadau kusimamia wenyewe kukusanya kupitia Taasisi zao badala ya COSOTA Ili yote kusaidia wabunifu kufanikiwa na Kazi zao.
"Ipo haja ya Kuanza kuchambua Sheria zilizopo na kanuni kuishauri serikali kuhusu mambo ya Muda mrefu tuliyokuwa tunaona kama.wabunifu Ili kutafita mwongozo wa namna hiyo"amesema Mwampembwa
Inocent Nganyagwa maarufu Ras Inno ni Mjumbe wa Bodi,Mwanzilishi na Katibu wa Mtandao wa Sekta Bunifu nchini Tanzania,amesema mirabaha hiyo Huwa inakusanywa katika maeneo yanayotumia burudani ikiwemo mahoteli,mabasi,vituo vya habari ambapo Fedha Hizo wanapewa wenyekazi zao kwa sababu ni sehemu ya faida za ubunifu wao.
"COSOTA imekuwa ikifanya vitu vingi Kwa wakati Mmoja kwa hiyo ilikuwa ni uhitaji wetu sisi wadau wa sanaa kwamba itenganishwe ibaki kuwa kama mdhibiti wa serikali lakini mabadiliko ya sheria yafanyike Ili iunde CMOs"amesema Nganyagwa
Naye Mwanawetu Mwani ambaye ni Katibu wa waandishi wa vitabu Tanzania amepongea hatua ambayo watu wa Muziki wamefikia hivyo akiishauri serikali kuanzisha pia Mfumo Kwa waandishi wa vitabu Ili nao waweze kunufaika na Kazi zao.






Post a Comment