DC MATINYI ASHIRIKIANA NA VIONGOZI WA BAKWATA KUFANYA USAFI.

............................

Na:Shalua Mpanda-TMC

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Mobhare Matinyi, asubuhi ya leo Septemba 23, 2023, aliungana na wananchi wa kata ya Kiburugwa katika tarafa ya Mbagala wilayani Temeke, kufanya usafi katika zahanati ya Kingugi.

Zoezi hilo la usafi liliandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika kata ya Kiburugwa chini ya Sheikh  Saidi Kiduka kiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Maulid ya Mtume Muhammad (SAW).

Akizungumza mara baada ya usafi huo na kuwashukuru uongozi wa BAKWATA, zahanati, kata, mtaa na wananchi kwa ujumla, Mhe. Matinyi alisema, "Ndugu wananchi tuendelee kufanya usafi kwa ajili ya mazingira yetu na afya zetu na zoezi hili liwe endelevu."

Naye Sheikh  Kiduka alisema usafi ni jambo muhimu katika jamii ambalo hata Mtume Muhammad (SAW) pia alilisisitizia na kumnukuu katika maneno yake akisema kwamba "Uislamu ni usafi".

Diwani wa kata hiyo, Mhe. Fatma Shija, naye alishhiriki katika zoezi hilo akiambatana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa ngazi ya kata na mtaa na hali kadhalika wenyeviti na watendaji wa kata na mitaa.

Baada ya zoezi hilo Diwani Shija alimchukua Mhe. Matinyi katika ziara fupi kumwonesha changamoto za miundombinu ya barabara, mifereji na mitaro katika kata hiyo ambapo Mkuu wa Wilaya alisema kwamba amejionea mwenyewe na amezipokea changamoto hizo.

0/Post a Comment/Comments