Mwenyekiti wa Bodi kituo cha uwekezaji Tanzania –TIC, Dkt Binilithi Mahenge amesema maboresho ya sheria yaliyofanywa na Serikali ikiwemo ile ya mwaka 1997 imesaidia kuongeza kasi ya uwekezaji Nchini hasa kwa wazawa.
Akizungumza Jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya ziara yake ya kutembelea kiwanda cha Plasco pamoja na cha mabati ya Alaf amesema maboresho mengine ni pamoja na kuzikusanya Taasisi za serikali zinazohusika na uwekezaji ili kumrahisishia mwekezaji anayetafuta vibali.
Pamoja na mengine Dkt Mahenge amewahakikishia wawekezaji wa ndani na wan je kuzitafutia ufumbuzi changamoto zao kwani serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya taasisi yoyote itakayohusika kukwamisha uwekezaji Nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji kituo cha uwekezaji Tanzania -TIC, Gilead Teri ameipongeza kampuni ya Plasco kwa uendeshaji wa kisasa ikiwemo matumizi ya teknolojia mpya ya utengenezaji bidhaa za plastiki.
Meneja Mkuu kampuni ya Plasco Ali Gulamhussein amesema licha ya mazingira wezeshi ya uwekezaji amependekeza maboresho ya sekta ya nishati ili kupunguza kuharibika kwa baadhi ya mitambo pale ambapo umeme unapokatika mara kwa mara.
Ziara hiyo ni ya siku mbili ambayo imeanza Jijini Dar es salaam huku septemba 22 inatarajia kufanyika Mkoani Pwani lengo ni kuhamasisha uwekezaji wa ndani.
.jpeg)
.jpeg)





Post a Comment