JIJI LA DAR KUWAFIKIA WAFANYABIASHARA KUPITIA MFUMO WA "TAUSI"

Baadhi ya Maafisa wa Biashara wa Jiji la Dar es salaam wakitoka huduma Kwa wafanyabiashara wa Kariakoo 
Afisa Biashara Mwandamizi Jiji la Dar es salaam Priska Mtendamema akieleza namna walivyowasogezea huduma karibu wafanyabiashara wa kariakoo Mtaa wa Raha na kuwapa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na biashara zao sambamba na kupata leseni na kulipia ushauri wa Huduma za Jiji.
..........................

NA MUSSA KHALID 

Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeanzisha Mfumo wa "Tausi' ili kuwarahisishia wafanyabiashara utendaji kazi popote walipo bila ya usumbufu wowote.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Biashara Mwandamizi Jiji la Dar es salaam Priska Mtendamema wakati walipowasogezea huduma karibu wafanyabiashara wa kariakoo Mtaa wa Raha ili waweze kupata ushauri wa kitaalamu kuhusiana na biashara zao sambamba na kupata leseni na kulipia ushauri wa Huduma za Jiji.

Amesema kuwa zoezi hilo limepata muitikio mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara kwani wamefika na kupata taarifa kuhusiana na biashara zao lakini pia kuendelea kuwaelimisha Ili kuweza kutambua kiasi wanachopaswa kulipia.

"Changamoto kubwa inayowakumba wafanyabiashara wengi wanakuwa busy na biashara zao Kwa kutokuwa na Muda wa kutosha kuweza kufuatilia kuweza kukamilisha taarifa sahihi kwa ajili ya Biashara zao Pamoja na kulipia huduma stahiki hivyo zoezi hilo litawafikisha huduma Kwa karibu"amesema Mtendamema

Aidha amesema kuwa kata ya Kariakoo ina wafanyabiashara wengi la watu wengi wamekuwa wapo busy na biashara zao hivyo jambo ambalo linawafanya kutokuwa na muda wa kutosha kwa ajili ya kufuatilia kukamilisha taarifa sahihi kwa ajili ya Biashara zao.

Amesema kuwa Mfumo wa "Tausi' umekuja mahususi kwa sababu ya kuwarahisishia wafanyabiashara utendaji kazi kwa kuwa wanawe kutumia maombi popote alipo bila ya kuwa na usumbufu wowote ila awe na vigezo vinavyohitajika.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wa kariakoo Kassim Suleiman Juma ambaye anamiliki Duka la Magic Touch mtaa wa Mafia na Jangwani ambao wamenufaika na zoezi hilo amelipongeza Jiji la Dar es alaam kwa kuanzisha Mfumo huo wa leseni kwani utawasaidia pia kuepukana na matapeli.

Amesema kuwa changamoto iliyokuwa inawakabili walikuwa wakiogopa kupata leseni feki hivyo Jiji kuwafata katika maeneo yao ya Biashara itawasaisia kurahisiaha huduma zao.

Vilevile Mfanyabiasha Andrea John amelishukuru Jiji kwa kuwa karibu na wafanyabiashara Huku akiwahamasiaha wafanyabiashara wengine kujitokeza kwa wingi Ili kupata Usajili na kuepukana na changamoto 

0/Post a Comment/Comments