Hayo yameelezwa jijini Dar es Salam na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mareva Tukai katika mkutano na waandishi wa habari na wahariri kuelezea taarifa ya utendaji, mafanikio na mwelekeo wa MSD.
Mkurugenzi mkuu huyo wa MSD amesema kwa Sasa Ununuzi wa Bidhaa za Afya kutoka kwa Wazalishaji wa ndani umeongezeka kutoka Bilioni 14.1 mwaka 2021/2022 hadi kufikia Bilioni 39.77.
Kuhusu Uwekezaji wa Viwanda vya Dawa pamoja na Uzalishaji wa Bidhaa za Afya, Mavere Tukai amesema Bohari ya Dawa imekusudia kuhusisha Sekta Binafsi kwa kutambua maeneo ya Uwekezaji wa Bidhaa za Afya za Kimkakati za Vidonge, Rangi Mbili pamoja na Vimiminika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la wa Hariri TEF, DEODATUS BALILE ameomba serikali na sekta binafsi kuendelea kushirikiana katika kuboresha sekta hiyo
Kwa Sasa Bohari ya Dawa nchini Tanzania (MSD) ipo kwenye hatua mbalimbali za Maboresho ikiwemo ile ya Kuimarisha Ufanisi wa Mnyororo wa Ugavi, kuimarisha mifumo ya Utawala na Usimamizi wa Vihatarishi.
Post a Comment