MKUTANO WA VYAMA VYA WAFUGA NYUKI KUFANYIKA NCHINI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki leo  jijini Dar es salaam wakati akizungumzia na waandishi wa habari akieleza nafasi ya Tanzania waliyoipata ya kuwa mwenyeji wa Kongresi ya 50 ya Shirikisho la Vyama vya wafugaji Nyuki Duniani inayotarajiwa kufanyika septemba 20-25 mwaka 2027 jijini Arusha
Baadhi ya waandishi wa habari Pamoja na wadau wa utalii waliohudhuria katika Mkutano huo
 ......................
 
NA MUSSA KHALID

Serikali imewataka watanzania na wadau mbalimbali kuwekeza katika ufugaji nyuki kwa kuwa sasa uzalishaji wa asali ni tani takribani elfu 32 tu wakati kama taifa kuna uwezo wa laki 138.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumzia nafasi ya Tanzania waliyoipata ya kuwa mwenyeji wa Kongresi ya 50 ya Shirikisho la Vyama vya wafugaji Nyuki Duniani inayotarajiwa kufanyika septemba 20-25 mwaka 2027 jijini Arusha

Waziri Kairuki amesema ametumia fursa hiyo kuwataka wadau wa ufugaji nyuki nchini kutumia fursa ya mkutano huo kuvutia wawekezaji na kuongeza tija katika ufugaji na biashara nzima ya mazao ya nyuki na utalii.

Aidha Waziri Kairuki amesema kuwa kwa Tanzania kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa APIMONDIA Tanzania inakwenda kuwa nchi ya pili Barani Afrika kupewa jukumu hilo kubwa la kuandaa kongresi hiyo tangu kuanzishwa kwa APIMONDIA miaka takribani 130 iliyopita. 

"Tumieni mkutano huu vizuri kwa kuongeza tija katika ufugaji na biashara nzima ya mazao ya nyuki, kuongeza wigo wa mashirikiano na taasisi mbalimbali duniani katika kuvutia uwekezaji katika sekta hiyo pamoja na kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za ufugaji nyuki hususani teknolojia na mbinu mbalimbali za kuboresha na kuendeleza sekta hii " Mhe. Kairuki amesisitiza. 

Awali akizungumza Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS0, Prof Dos Santos Silayo amesema kuwa wamechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaweka wafugaji wa Nyuki pamoja.

Amesema wamechukua hatua mbalimbali kuhakikisha sekta ya Utalii inakua kwa kuwaruhusu wananchi wanaoiahi karibu na misitu ya uhifadhi kuingia na kufuga nyingi bila ya malipo

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika jiji la Arusha hivyo Mstahiki Meya wa jiji hilo Maximilian Irange amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaboresha maendeleo ikiwemo kuweka taa katika barabara mbalimbali.

Katika Mkutano huo pia amehudhuia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Mkurugenzi wa Huduma za misitu na wadau mbalimbali.

APIMONDIA ni Shirikisho la Umoja wa Vyama vya Wafugaji nyuki Duniani lililoanzishwa mwaka 1895 nchini Italia huku. Tanzania ilijiunga katika shirikisho hilo mwaka 1984 ambapo Tanzania kwa mwaka huu nchini Chile iliibuka kuwa mshindi wa kinyanganyiro cha kuandaa Mkutano wa 50 mwaka 2027 ni Tanzania.

Imeelezwa kuwa mkutano huo unakadiriwa kushirikisha wadau zaidi ya 6,000 toka mataifa mbalimbali dunia hivyo Tanzania kuwa mwenyeji wa kongresi hiyo kunatarajiwa kuleta manufaa makubwa ya kuchochea ukuaji wa sekta ya nyuki na uhifadhi, kuongeza mchango wa sekta katika pato la taifa, kuchochea utalii kwa ujumla nchini na kuvutia uwekezaji wa viwanda na teknolojia katika sekta ya ufugaji nyuki.

0/Post a Comment/Comments