Baadhi ya wakuu wa idara wa Kampuni ya Bima ya NIC wakifuatilia kikao hicho wakati kilipokuwa kikiendelea.
Baadhi ya Wahariri na waandishi na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya (NIC) Dkt. Elirehema Doriye wakati akizungumza na TEF.
*********
Imeelezwa kuwa ili kuwafikia watanzania wengi na kuendelea kutoa huduma za kidijitali, Shirika la Bima NIC INSURANCE limekusudia kuwekeza zaidi katika Tehama.
Mkurugenzi Mtendaji NIC, Elirehema Doriye amesema hayo leo na kuongeza kuwa wameendelea na mpango mkakati katika kutoa elimu juu ya huduma ya bima.
Pamoja na kuwa na dira yenyewe ufanisi, weledi, tija na maadili yenye msingi amesema kuwa ndiyo muongozo wao wa kufanikiwa katika uhuru wa kufanya kazi na biashara.
Amesema kuwa kulikuwa na ongezeko la faida kwa mwaka 2019/2020 ilikuwa Sh bilioni 33.65 hadi Sh bilioni 63.21 2021/2022 sawa na asilimia 43.91 kwa mwaka wa fedha.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (TEF) Neville Meena pamoja na kushukuru shirika hilo pia amewasihi wahariri na waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele katika kutumia bima hiyo kama msaada wa dharura wawapo maeneo ya kazi.
Aidha amewasihi mashirika binafi na ya umma kuweka mkazo katika huduma hiyo ya bima ambapo wengi wao wamekuwa hawana elimu ya kutosha juu ya elimu ya bima katika jamii ya kitanzania.





Post a Comment