RASMI MABASI YA ABIRIA KUSAFIRI SAA 24 TANZANIA

 




*******

Serikali imeruhusu mabasi ya abiria kufanya usafirishaji kwa saa 24 kuanzia Oktoba 1,2023, baada ya kuweka zuio kwa takriban miaka 29.

Zuio hilo liliwekwa mwaka 1994 la kuzuia mabasi kusafiri usiku, lililosababishwa na matukio ya utekaji wa mabasi uliohusisha uporaji na udhalilishaji wa abiria, ajali mbaya za mabasi zilizogharimu maisha ya watu na wengine kupata ulemavu wa kudumu.

Akiongea na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini amesema, Serikali imefikia uamuzi huo baada kuboresha miundombinu ya usafiri husuan barabara kuu na barabara za mikoa, na hivyo  kuifanya nchi kuwa moja ya nchi zenye usafiri wa barabara unaoaminika na bora.

Aidha, amesema wafanyabiashara wanaomiliki mabasi hayo ambao wako tayari kufanya safari kwa saa 24 ni muhimu wakazingatia  Sheria, Kanuni na Miongozo kuhusu usafiri na usafiri wa abiria.

“ Katika kutekeleza uamuzi huo wenye nia njema madereva wa mabasi wanapaswa kuthibitishwa na LATRA kwa mujibu wa miongozo iliyopo. LATRA inapaswa kutoa ratiba za safari za saa 24 kwa kushirikisha watoa huduma, na kuhakikisha Mfumo wa VTS na kituo cha mawasiliano vinafanya kazi wakati wote.” amesema Sagini.



0/Post a Comment/Comments