Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Selestine Gervas
Kakele wakati akifungua kikao cha kutoa maoni kuhusu rasimu ya sera ya Taifa ya
Tehama ambacho kimewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo watu wenye changamoto
za ulemavu ambacho kimefanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wadau
ambao wameshiriki katika kikao cha kutoa maoni kuhusu rasimu ya sera ya Taifa
ya Tehama ambacho kimewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo watu wenye
changamoto za ulemavu ambacho kimefanyika leo jijini Dar es salaam.Na Mussa Khalid
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imewataka wadau mbalimbali kushiriki katika utoaji wa maoni kuhusu rasimu ya sera ya Taifa ya Tehama kwani inamchango mkubwa katika kuboresha maisha ya watanzania.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Selestine Gervas Kakele wakati akifungua kikao cha kutoa maoni kuhusu rasimu ya sera ya Taifa ya Tehama ambacho kimewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo watu wenye changamoto za ulemavu.
Kakele amesema moja ya taratibu za uandaaji sera ni pamoja na ushirikishwaji wa jamii katika kujadili sera hiyo kwani itasaidia kutatua changamoto Kwa watu wenye makundi anuani katika matumizi ya Tehama.
"Tumekuwa na sera ya Tehama ya Mwaka 2016 hivyo ni Muda mrefu umepita na Tehama ni kama kiumbe kinachozaliwa ,na kukua kulingana na wakati hivyo tumeona kwamba ipo namna ya kuanza kufanya marejeo"amesema Kakele
Amesema kuwa tangu wamekuwa na utaratibu huo wamekuwa wakikutana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanatoa mitazamo yao kuhusiana sera ambayo inafanyiwa mapitio.
"Yote haya tunayoyafanya ni katika mawanda mapana ya mradi wetu wa Tanzania ya kidigitali ambapo moja ya mpango ni maboresho ya sera hivyo tutoe maoni yetu ambayo yatakwenda kujenga zaid"amesema Kakele
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa kikao hicho,Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dar es salaam Salum Matimbwa na Bi Fatma Kange wamesema ni wajibu kwa Wizara kuona namna ya kuhusisha maoni yao katika sera hiyo ili iweze kuleta tija.
Pia Halima Mhando kutoka Chama cha Wachimbaji wanawake Tanzania ameipongeza hatua hiyo kwa kuwa miongoni mwa washiriki katika kuhuisha sera kwani itakwenda kuwaongezea soko katika nyanja mbalimbali huku Ernest Kimaya Mwenyekiti wa Shirikisho la Vya vya watu wenye ulemavu Tanzania amesema katika maisha ambayo wanayaendea ni muhimu kuwa na muelekeo mzuri kwa Tehama hivyo watahakikisha wanatoa mawazo yao ili yaweze kufanyiwa kazi.

Post a Comment