Timothy Marko
SERIKAli imewataka wanawake na vijana kuchangamkia Programu ya imbeju inayoratidiwa na Benki ya CRDB ilikuweza kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza katika kongamano liliowakutanisha wajasiliamali wanawake na Vijana katika wilaya ilala nakuratidiwa na Benki ya Kibiashara ya CRDB mapema hii leo jijini Dar es Salaam Waziri wamaendeleo ya jamii jinsia na Makundi Maalum Dk.Dorothy Gwajima amesema Serikali imelenga kuwapatia vijana wanawake wajasiliamali Vitambulisho vya kidigitali ilikuwawezesha kupata Mikopo kwenye Mabenki.
"Hatua zinazo chukuliwa na Serikali nikuwa inua wanawake na vijana kiuchumi nipamoja kuwawezesha Makundi haya kuzifikia fursa za kiuchumi".Alisema Waziri wa Maendeleo yajamii ,jinsia na Makundi Maalum Dk Dorothy Gwajima.
DK.Gwajima alisema kuwa katika ripoti ya Mwaka 2022 ya Sensa ya watu na Makazi ilionesha kuwa wanawake nchini ni Asilimia 52 wakati vijana ni Asilimia 43.
Alisema Mikopo ya Asilimia 10 ya Halimashauri inayotolewa na serikali imehamishiwa kwenye mabenki ya kibishara ilikuwawesha wanawake na vijana kupata Mikopo hiyo.
"Ili wafanyabishara kuweza kupata fursa mbalimbali za kibiashara kwa bidhaa zenu nivyema mkaziwekea backord bidhaa zenu ilikuweza kutambulika kimataifa".Aliongeza Waziri wa Maendeleo ya jamii Dorothy Gwajima.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Abdul Majid Nsekela amesema kuwa kundi la wanawake na Vijana nimuhimu katika kujenga uchumi.
Alisema Benki hiyo imekuwalikiwasadia wanawake na Vijana katika kuwapa Elimu yaBiashara sambamba na Mitaji .
"Benki ya CRDB imetoa Mikopo ya trioni 3.4 kwa vijana na wanawake"Alisema Mkurukugenzi wa Benki hiyo AbdulMajid Nselekela.
Nseleka ameongeza kuwa kupitia programu ya imbeyu imeweza kutoa zaidi bilioni 5ilikuwezesha wanawake naVijana .
"Wafanyarabishara na Vijana niwaombekuchangamkia Mikopo hii ya imbeyu ".Alisema Nsekela .
Wakati huo,Naye Mkurugenzi wa Vikoba na Mnufaika wa Programu ya Imbeju Semeni Gama amesema imewawezesha kuwapatia wajasmali zaidi mikopo ya Shilingi milioni 270.
Alisema Kupitia mikopo hiyo imewawezesha wajasmali kuweka Akiba zao kwa gharama ndogo na kuwapatia mitaji ya biashara.
"Witowangu kwa wafanyabiashara waweze kurejesha mikiopo hii kwa wakati".Alisema Mnufaika wa program ya imbeju Semeni Gama.

Post a Comment