TANESCO WAPEWA SAA MBILI KUTATUA KUKATIKA KWA UMEME UBUNGO ONE

 


Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akizungumza na waadishi wa habari wakati alipotembelea makao makuu ya Tanesco



                                ******

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ametoa saa mbili hadi Sita kwa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, kuhakikisha wanatutua tatizo la kukatika kwa umeme katika Kituo Cha uzalishaji wa umeme ubungo one.

Kiongozi huyo ametoa maagizo hayo jijini Dar es Salaam leo, wakati akitembelea makao makuu ya shirika hilo yaliyoko Ubungo kwa ajili ya kuangalia hali ya uzalishaji wa umeme katika kituo cha ubungo one na ubungo two.

Baada ya ziara yake amesema Kwenye Kituo cha ubungo two mashine za kizalisha umeme ziko tatu lakini moja haifanyi kazi na ipo kwenye matengenezo na inauwezo wa kizalisha megawati 43 kila moja. 

Ameongeza kuwa kwenye Kituo Cha Ubungo one mashine zipo 12 lakini sita kati yake ziko kwenye matengenezo na kwamba muda wotewote zitakamilika na kurejesha uzalishaji kama awali. 

Amesema adhima ya Serikali ni kuona watanzania wanapata umeme na kukamilisha matengenezo hayo ndani ya miezi sita, akisistiza kuwa kama marekebisho hayo yatafanyika kwa wakati tatizo la umeme litakwisha.

0/Post a Comment/Comments